Pamoja na ukongwe wa CCM, Januari Makamba ametuonesha udhaifu wa mfumo wa utawala

nasisitiza kuna watu baba zenu walitakiwa kutoa nje, na siafu na sisimizi wakala yale makamasi
 
Maajar ilikuwa enzi za JK. Kipindi kile Dowans na Tanesco
Bora hata hao akina mchechu na mafuru maana hawakuwahi kujihusisha na Tanesco
Kuamini kauli za wanasiasa ni shida kweli, wao huwa wanaangalia interest zao tu. So kwa upande wangu naona kuwa kashfa zao zaweza kuwa kweli au famba pia.
 
Watu hao watakuwa na maslai binafsi ya tanesco hii haikubaliki tunahitaji katiba mpya tuondokan na ccm
 
Angalia watakaoiendesha Tanesco Mafuru Tanesco- Mtu ambaye inasemekena alifanikisha GSM kusomba pesa za NBC kununulia magari ya mizigo bila kulipa deni. Mchechu –Aliyejinufaisha badala ya kuinufaisha NHC. Majaar –mdanganyifu wa kisheria, Tanesco ikaingia matatani hadi leo. Kubwa zaidi, imekuwaje wote hawa kukubali uteuzi huo wakati wakijua umma wa kitanzania hauna imani nao? Hata kama walisingiziwa, je, hawana busara za kujiondoa?[emoji23]

Hii inaitwa bucha limekabidhiwa mafisi
 
Nilivyoona teuzi ya B.B kuwa RC nikajua tayari hakuna jipya kwahiyo yanayoendelea sasa wala sishangai
 
Mkuu

Kilichofanyika sio bahati mbaya au nzuri ila ni mkatati maalum, kwa sababu maalum , kwa muda maalum na malengo maalum wala usiumize kichwa bure ni kawaida kwa nyumba za vijijini usiku mwanga ukizima majoka aina ya swila kujongea ndani ya nuumba yakivizia kugonga kuku na kula mayai ya kuu hilo ndilo linalofanyika.

Hizo ndizo dharau ya utawala kutozingatia sheria na kuupuza maoni ya wananchi wanaofahamu zaidi kuhusu maovu ya viongozi.

Kwa sasa mwenye nguvu ya kiuchumi ndio anabebwa bila kujali madhara ya uamuzi unaofanyika.

Mwombeni Mungu atawanusuru na madhila zaidi.
 
Mataga enzi zenu zimeisha, acheni kuhangaika kama kuku anayetaka kutaga.
 
Unao ushahidi, au ndiyo "inasemekana?"
 
Kwa maana hiyo hakuna ufisadi wowote hapa nchini
 
Hauko sahihi. Hata mimi Magufuli kuna mambo nilikuwa namkubali ila kuna mengine alifanya vibaya sana sana. Na ndiyo hayo watu walikuwa wanamlalamikia. Kwanza kama angekuwa amekubali tukawa na katiba mpya baada ya uchaguzi wa 2020, haya yote yasingetokea kabisa. Mimi tangu zamani mama Samia nilijua ni kimeo na siku likitokea la kutokea nchi itarudi kwenye mikono ya mafisadi kushinda wakati mwingine wowote.
 
Kumuweka tu Maajar ambae aliisaidia Dowans kuwaliza Tanesco ni Jambo la ajabu sana.
Bado najiuliza ina maana viongozi wetu hawana kumbukumbu?
Kama tanesco walikua na wansheria dhaifu angefanyeje
 
Nilivyoona teuzi ya B.B kuwa RC nikajua tayari hakuna jipya kwahiyo yanayoendelea sasa wala sishangai
Hakuna kitu kinacholevya kama madaraka. Mtu akishakalia kile kiti anajiona yeye ni sawa na Mungu na pengine amemzidi hata Mungu. Nina uhakika kabisa team Chato ingejua kitakachotokea lazima kungekuwa na mabadiliko makubwa ya katiba na mama asingekuwa ndiye mrithi. Kila nikikumbuka kipindi cha Magufuli, watu wa timu Msoga walivyokuwa wanajuta na kuilaani hii katiba nashangaa sana wanasiasa walivyo. Sasa hivi wameshajisahau na hawaoni tena ubaya wa katiba ila wanajipanga namna ya kula. Ila na wao wamesahau kuwa kesho linaweza kutokea jingine ambalo hawakuliwaza kabisa na madaraka yakaenda kwa wengine.
 
Kumuweka tu Maajar ambae aliisaidia Dowans kuwaliza Tanesco ni Jambo la ajabu sana.
Bado najiuliza ina maana viongozi wetu hawana kumbukumbu?
Wamewekwa watu wenye maslahi ktk sekta ya nishati. Hawajateuliwa bahati mbaya. Wamerudi KWA Kasi kuitafuta nchi.
 
Kuamini zile kauli za Jiwe ilibidi uwe na uwezo kama wake au chini yake kama wewe.
Kwani hadithi za akina Mafuru zilianza wakati wa Magufuli? DOWANS scandal ilianza wakati wa Magufuli? Huna hata akili ya kujiuliza yalianza lini! You seem stupid!
 
Jamani tuache uongo,mwenye ushahudi auweke sio tuhuma za kupuuzi kama hizi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Nchi hii haina watu wapya zaid ni wale wale mfano ktk hili la teuzi! Inashangaza na kushindwa kuelewa ni kivipi wanashindwa kuwapata watu ambao wapo katika taasisi nyingi tu, tuendako ndiko turudiko sijui tutafika lini
 
Kwani hadithi za akina Mafuru zilianza wakati wa Magufuli? DOWANS scandal ilianza wakati wa Magufuli? Huna hata akili ya kujiuliza yalianza lini! You seem stupid!
Wapi nimesema zilianza kipindi cha Jiwe? Una akili kweli wewe? Au hujui hapo kuna kipindi/awamu zaidi ya moja?
Pathetic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…