Pamoja na ukongwe wa CCM, Januari Makamba ametuonesha udhaifu wa mfumo wa utawala

Nchi huliwa na wenye meno sio vibogoyo.
Actually, nchi hii imegeuka uchi. Hata vibogoyo wanakunywa tu! Tumewezaje kuruhusu elimu za hapa na pale ndo zinaongoza nchi?
 
Hii yote ni kunyanganywa kitumbua mdomoni. Tulia dawa iingie, nchi inatakiwa iongozwe kistaarabu sio mabavu na maonevu. January tuonyeshe njia. Waache walie lie tutolee tatizo la umeme achana na porojo za mitandao wanalia ndio walee. You have gas at kinyerezi ongeza generators za umeme ondoa tatizo la umeme tuachane matatizo za umeme.
 
Huyu mama alikuwa hadi balazo marekani , mara mwenyekiti wa vodacom huko hakutosheka tu mpaka leo anataka madaraka
Shida siyo madaraka, wizi uko kwenye damu kwa mama huyu. Bahati mbaya anasukumwa na wengi wanaoiibia nchi hii. Kila familia ya wanasiasa in njaa kali ya pesa za umma.
 
Totally ignorant! wanachojadili kingine, wewe unamshangilia Januari. Hiyo elimu yake ya conflict resolution iondoe tatizo la umeme? Kuna mambo yanahitaji a lot of brain power. Hapo huna mtu wa aina hiyo, boss!
 
Mahakama gani enzi hizo za ufisadi kutawala. Hadi majaji walikua wanahongeka.
 
Tatizo la ufisadi watanzania mkuu,unamtandao mrefu,wakuu wa nchi ndo wanafanya hayo kwa kuwatuma wateule wao.
Kesi ikianza kufuatiliwa ,anatakiwa Mkuu wa nchi wa wakati ule afike mahakamani kujibu hizo tuhuma.
Kwa katba iliyopo na CCM,hiki kitu hakiwezi tokea.
Nikuulize tu mkuu,unadhani Richmond ilikuwa feck? Lakini alitolewa sadaka Edward,ilikuficha ufisadi.
AFRICA TU NDO MWIZI ANATENGULIWA MADARAKANI NA KUACHWA.
KAMA ZINGELIKUWA NI SIASA ZA MAJI TAKA LAKINI HAWAIBI,TZ TUSINGELIKUWA WAKUSUBILI MPAKA MSAADA WA KUJENGA VYOO NA VISIMA KWA WANANCHI. AU KUSUBILI TOZO KUJENGA BARABARA ZA VIJIJINI. INAUMA SANA NA KUKERA.
 
Hawa akina Mchechu, Mafuru, Mramba, nk ni vichwa vilivyoogopwa na Mwendazake na kuondolewa kwa chuki binafsi hapa mama amelamba dume kuwarudisha.
 
Hawa akina Mchechu, Mafuru, Mramba, nk ni vichwa vilivyoogopwa na Mwendazake na kuondolewa kwa chuki binafsi hapa mama amelamba dume kuwarudisha.
Kwa hiyo siku wakifa TZ imekufa? Umefanikiwa kuwajua majina yao kupitia ufisadi wao wakati wa Kikwete, lakini kuna watu nchi hii ni wazuri na wana maana kubwa kuliko hao watu hopeless. Ukishakuwa mwizi, that's!
 
Mahakama gani enzi hizo za ufisadi kutawala. Hadi majaji walikua wanahongeka.
Siyo tu walihongeka, hata bei zao tulizijua. Ukiwa na kesi ya mauaji milioni 50, unajiondoa.
 
Totally ignorant! wanachojadili kingine, wewe unamshangilia Januari. Hiyo elimu yake ya conflict resolution iondoe tatizo la umeme? Kuna mambo yanahitaji a lot of brain power. Hapo huna mtu wa aina hiyo, boss!
Wailotoka kuna watu wa aina hiyo? Waache watekeleze kazi zao. Kuingiliwa TANESCO na wanasiasa ndio waliowaletea matatizo yote haya, hasa kipindi cha crissis. Wamechukua watu na taaluma zao za kuendesha mashirika binafsi ili wachangie wakiwa pamoja na wataalamu wa TANESCO hiyo ignorance imetoka wapi? Ulitaka waziri awe mwanasheria kama aliekuwepo? Je day to day opearations hufanywa na Waziri? that is why you need other brains hata Waziri kugundua uozo uliokuwepo nao ni upeo.
 
Kwa hiyo siku wakifa TZ imekufa? Umefanikiwa kuwajua majina yao kupitia ufisadi wao wakati wa Kikwete, lakini kuna watu nchi hii ni wazuri na wana maana kubwa kuliko hao watu hopeless. Ukishakuwa mwizi, that's!
Kumbuka hao ndio waliopaisha NHC na Tanesco kabla ya kuvurugwa na wateule wa Magufuli ambao wengi ni wapwa zake.
 
This is Simba bwana,ndo Tanzania hiyo watanzania sisi kazi yetu Ni kulalamika tu.hatuchukui hatua
Na majungu, kama mna uhakika ni wezi wafungulieni kesi jinsi haina ukomo halafu watawapa hela ili mfute kesi si na nyie ntakuwa mmepiga hela, maneno mengiii🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…