Pamoja na ukuta mrefu na JWTZ kulinda Mererani, nani bado wanaiba madini yetu?

Kwanini ule ukuta usiende chini zaidi kupita hayo matundu ya mahandaki
 
Hivi askari coplo au sagenti mnamlipa mshahara wa laki 5 kwa mwezi alafu kwa siku apewe milioni 200 au 100 au 50 tuu aachie mzigo upite atakataa?hata kama ni mimi nakataaje kwa mfano
 
Through
1) Mikataba
2) kupitia palepale getini - Unaiba mawe 20 unawaachia wengine (walinzi etc) mawe matatu.
 
Mtu ana manyota mpaka anaelemewa halafu hana hata senti mfukoni kwanini asiwe mwizi, majeshi na watumishi wa umma wamebakwa sana kwa miaka hii mitano iliyopita
 
Ninyi mna amini kabisa ukuta ndio unaweza kuzuia madini kupitishwa? kwani madini ni gari kusema ukifunga geti haliwezi kupita?

Tujifunze hata kwa private entities kama GGM kule kuna ulinzi mkali sio wa kawaida, na security checks za kutosha, bado wakuu wakijipanga vizuri wanapiga mzigo hapa na pale (japo kwa uchache)

Labda atusaidie 24/7 kinachofanyika huko mererani ni kipi, eti tweenty4seven hebu tupe habari za huko basi, kina nani wanafanya haya?
 
Mauzo kabla ya ukuta na baada ya ukuta yakoje?

 
Ivi yule morel alichimba na kupata kweli yale madini au zilikuwa sarakasi tu za yule mzee??
 
KAMA JIWE ANGEAMBIWA KUWA INGAWA ALITUMIA GHARAMA NYINGI KUJENGA UKUTA NA KUTOA SIFA NYINGI KWA JESHI KWA KULINDA MIGODI YA TANZANITE LAKINI MADINI BADO YALIKUWA YANAIBIWA ANGEONEKANA MJINGA NA HILO LISINGEMPENDEZA MPENDA SIFA YULE!!! ANGEWAKA MOTO!!
Alipigwa mchana kweupeeeeee
 
Ndiyo maana Sukuma Gang wamepanic mbaya
 
Unajua hii ni kashfa kubwa sana inayohitaji uchunguzi wa kipekee. Aliposema vile camera ikawaonyesha wakuu wa vyombo vya UU, wamevimbisha sura kweli kweli.

Nadhani katika mambo yote mabaya yaliyosemwa mpaka sasa katika hizi wiki mbili kuhusu utawala wa mwendazake, hii inashika nafasi ya kwanza au ya pili.
 
Kikubwa walijenga kuzuia nini?

Na ukuta huo una security level ipi?

Na ukuta huo unalindwa na watu wenye utaalam wa aina gani?.
Itoshe tu kusema biashara ya madini ina fake nyingi huwezi kulinda kwa kufoka foka kama mwehu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…