Haya mambo Ndiyo Yale yale ya kushow off , huyo kiba kauza sana wimbo wake wa aje mwaka Jana kwenye mitandao na hasa audio, kaingiza pesa nzur mkataba wake na sonny , show zake za nje ulaya na marekani, juz juzi tu kapiga pesa ndefu sana huko kenya kwenye kampeni za akina odinga hasa Mombasa ( gavana joho )
Ukija kwenye video ( account za VEVO msaan kule analipwa kwa view zake ) ishu hapa ni mmoja anapenda kujionesha na mwingine ni kimya kimya hata kiba ana jumba lake la maana lipo pale tabata sema ni vile tu haongei , kampuni ya Rockstar ni yake sasa wanauza nyimbo na ishu zote za entertainment Africa lakin hujawahi kusikia akijisifu hata siku moja
Mfano mzuri wasaani wenye pesa ndefu afu wapo simple tu
Yupo A.y huyu ana pesa ( na ndiyo mtu wa kwanza kumtengenezea connection mond na akina davido ) huyu anamilik kipind cha mikasi na ana project zingine lakin huoni akijisifu hata siku moja
Mwisho niseme wote ni vijana na ni wapambanaji ila kila mtu na makuzi yake na tabia yake ya matumiz ya pesa
Wengine kwetu ni somo kuwa upate pesa upige kelele na show off au ukae kimya tu
Sent using
Jamii Forums mobile app