Pamoja na usomi wangu siachi matambiko na mila ng'oo

Ila usiende na watoto wako waache wafike umri wa kujitambua ndio uwaambie matambiko waaingie wenyewe.

Kifupi weww ni mpumbafu unaejidai kujua kafie mbele wewe kama wewe watoto waache hujui kuhusu hayo mambo uko mjinga na gizani sana.
Mbona povu..jibu hoja acha kutukana esta.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mizimu ni shetani kuvaa sura au uhusika wa wazee wa ukoo.
Roho ikifa haibaki duniani either kuzimu au peponi ikisubiria siku za hukumu.
Ibada ni sehemu mbili either kwa Mungu au Shetani.
Uliiona roho iko mbinguni??

#MaendeleoHayanaChama
 
Akili ya mtu inawezwa ikashindana na elimu na dini na ikashinda hivyo hatukushangai. Kuna watu wamesema kweri kweri lakini nature yao imeishinda hiyo ilimu yap
 
Dini ni mfumo.
Mfumo wa kumtafuta Mwenyezi Mungu.
Mungu ni mmoja hakuna Mungu tofauti na yule alieumba ulimwengu tunaoishi.
Na pia shetani yupo, anaishi ndani ya kila mmoja kama ilivyo Mungu anaishi ndani yetu (Twin souls), a very complicated phenomenon na inahitaji kujifunza ili kuweza kulithibitisha hilo.
Na pia katika kujifunza nimefahamu ya kuwa kifo sio mwisho wa safari, kwamba.. sasa ndio unaenda kukutana na Mungu kama wengi wanavyo amninishwa. Ukifa unaingia kwenye dimension ya juu na unakuwa na nguvu kubwa za kiroho, na utaweza ku interact na dimension ya chini uliyotoka kama ulikuwa na uwezo mkubwa wa kiroho wakati unakufa. So hii inatoa maleezo juu ya lile swala la kuwaomba ma babu/wazee wa jadi waliotangulia ili waweze kutoa hint/muongozo juu ya jambo fulani, lakini haimaanishi kuwa ndio tunatakiwa tuwaabudu wao.
Kila jamii ilikuwa na mfumo waliouamini katika kumuomba Mungu. Waafrika tulikuwa na dini zetu, wazungu dini zao, wachina, wahindi etc. Kilichotokea ni kwamba tuliaminishwa na walio tutawala kuwa dini zetu sio sahihi, tuliaminishwa kuwa mababu zetu na wazee wetu wa jadi walikuwa wakiabudu miungu/mashetani. Isingekuwa rahisi kututawala kama wasingefuta kile tunachokiamini.


Kuhusu Jesus Christ:
Kuna kitu watu wanachanganya sana. Na kuna ambao mpaka leo hudhani ya kwamba 'Jesus Christ' ni jina la myuda aliyeishi nyakati hizo kama ilivyo kawaida ya mtu kutambulika kwa majia mwili.
Uhalisia ni kwamba 'Christ' is not a person, 'Jesus' was a person. Christ ni jina lingine la God Christos, likimaanisha the Fire God.
Jesus-Iesus-Zeus aliitwa 'Jesus Christ' baada ya ku_incarnate the cosmic christ.
Christic principle ipo kwenye kila dini ingawa wengi hawalifahamu hilo, na ndio maana tunasema wote tuna muabudu Mungu mmoja.
Hakuna tofauti kati ya Chriatian priest na Mohammedan priest, wote wapo kwenye kapu moja. Vivyo hivyo kwa waafrika, wachina, wahindi, wagiriki, egyptians etc. Christ is cosmic and universal!

Kwa
Egyptians, Christ alikuwa Osiris.
Hindus, Chrishna ni Christ.
Chinese, Fu Hsi ni Christ.
Greeks, Christ anaitwa Zeus, Jupiter the father of Gods.
Germanic edda, Christ ni Balder.
Afrika pia naskia tulikuwa tuna black Christ ingawa sijafanikiwa kufahamu alifahamika kwa ma/jina gani. Na hapa ndipo naiona nguvu ya wakoloni walio tutawala, walipambana kuhakikisha wanatuacha wakavu! Wakavu kiuchumi, wakavu kimaarifa na mbaya zaidi wakavu kiimani!
That's why utakuta mpaka leo tunajifunza maarifa ambayo yanakuwa ni magumu kuendana na uhalisia wetu. Utakuta leo mtu anajifunza chinese meditation kesho kutwa ana recite krisha mantra yaani inakuwa ni vurugu tupu. Sipingani na watu kujifunza maarifa tofauti yenye manufaa, ila nadhani kuna tofauti kubwa ya matokeo kwa wewe utakaye recite 'krisna mantra for success' na yule atakaye enda kijiji kwa babu zake kuomba msaada pale alipo kwama.
All in all we have free will, kila binadamu ana uhuru wa kuchagua kipi kinamfaa.


Hiyo hapo juu ni image pekee yenye uhalisia kuhusu muonekano wa Jesus Christ kwa wale wanaoamini katika Yesu alietokea kwenye kabila la Yuda, na ilipatikana baada ya Sultani wa uturuki kuikabidhi kwa pope Innocent VIII kama ransom ili kaka yake aliyekamatwa na wakristu wa miaka hiyo aweze kuachiwa.
 
Mungu akusaidie umjue Yesu ili uekwepe moto wa milele
Soma kwanza na ujifunze kwa nini Waisrael na wayahudi sio wakristo na hawamkubali Yesu wakati mnasema alizaliwa kule na wao ndio ndugu zake kabisa. Yaani ni babu yao kabisa. Wewe Kalimanzila kutoka Kigoma ndo unajidai unamjua sana Yesu na atakukomboa[emoji3][emoji3]


Waafrika hebu tuache uzwazwa
 
Hiyo picha uongo..

#MaendeleoHayanaChama
 
Kabla sisoma chochote naami maisha yko ni mazuri baada ya kulitambua hilo na kulifanyia kazi...watu wanataka waganga wa kuwapa utajiri lkn wanashindwa kufanya vitu vdogo kama matambiko ambayo ndio ufunguo mkubwa wa mafanikio
 
Kabla sisoma chochote naami maisha yko ni mazuri baada ya kulitambua hilo na kulifanyia kazi...watu wanataka waganga wa kuwapa utajiri lkn wanashindwa kufanya vitu vdogo kama matambiko ambayo ndio ufunguo mkubwa wa mafanikio
Nahitaji maelekezo ili mwaka huu na mimi nianze rasmi..kila siku hua naamini katika mila zetu sema nmekuta kizazi tayari kiko brainwashed na hizi dini za kuja..nisaidie pa kuanzia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nahitaji maelekezo ili mwaka huu na mimi nianze rasmi..kila siku hua naamini katika mila zetu sema nmekuta kizazi tayari kiko brainwashed na hizi dini za kuja..nisaidie pa kuanzia.

#MaendeleoHayanaChama
Nenda kijijini kwenu tafuta wazee wa kimila waeleze dhumuni lako... lkn pia anza kuwatembelea ancestors wako na kujenga ukaribu nao
 
Hapa ndo Waafrika tunakosea kabisa. Tunajidai kujua wakati hatujui. Mtu unaamka tu unawaza vitu kichwani ,unaviandika na unataka tuvifuate
Angalau ungefanya utafiti kuhusu unachokiita mizimu ya kiafrika walau utupe sample uliyotumia kufikia conclusion.
Umeishia tu kushambulia imani za watu. Kama imani yako ni bora kuliko zingine, ungeonyesha ni wangapi wamefanikiwa na walifanyaje
Imani nyingi za kiafrika ni za kinafiki,kuoneana kijicho na wivu na kulogana pia
Mizimu ni majini/mashetani. Kutoa kafara ni kulisha mizimu. Haiwezekani mtu akishakuwa marehemu ndo awe na nguvu ya kutuletea mafanikio , mtu ambaye alifariki bila hayo mafanio yoyote. Leo afe aitwe mzimu atuletee utajiri.
Narudia tena ,mizimu ni mahetani wanajifanya ni ndugu zetu waliokufa
Rejea shetani alichosema kwa Yesu, kuwa mali na fahari ni mali yake ,ukimsujudu unapewa mali. Kwa hiyo ukitoa kafara ,hiyo ni umemsudu shetani ,atakuzawadia mali
Fanyakazi kwa bidii huo ndo utajiri halali unapatika
 
Mkuu endelea kuwa na imani yako,ila hivi hujiulizi kwanini watu ambao wanaishi maisha yao ya asili ndo wanaishi miaka mingi mtu kanisa halijui maombi anaomba babu zake na mungu anambariki
 
Shida ni watu kuchanganya dini. Mkristu au Muislamu lakini hapohapo kavaa hirizi au anatambika. Ni vema mtu akafuata dini moja tu, au ya kimila au ya kuletwa.
 
Shida ni watu kuchanganya dini. Mkristu au Muislamu lakini hapohapo kavaa hirizi au anatambika. Ni vema mtu akafuata dini moja tu, au ya kimila au ya kuletwa.
Wakristo wanakatazwa kuombea wazee wao..ila kutwa kuombea wazee wa kizungu kwa mlango wa watakatifu..hapa kiukeli tulipigwa pakubwa


#MaendeleoHayanaChama
 
Ukikua utatambua ujinga wako.
 
Wakristo wanakatazwa kuombea wazee wao..ila kutwa kuombea wazee wa kizungu kwa mlango wa watakatifu..hapa kiukeli tulipigwa pakubwa


#MaendeleoHayanaChama
Huenda ikawa hivyo. Ndio maana hili mtu akiliona kihivyo ni bora abaki kwenye dini za kimila moja kwa moja. Asiwe nusu mkristu/muislamu na nusu wa kimila.
 
Huenda ikawa hivyo. Ndio maana hili mtu akiliona kihivyo ni bora abaki kwenye dini za kimila moja kwa moja. Asiwe nusu mkristu/muislamu na nusu wa kimila.
Bora tuutafute ukweli mana mimi naamini waafrika dini zao zilikua zina Nguvu sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naomba mstari wa kwenye biblia unaonsema tuwakumbuke wafu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…