Tumieni angalau hoja defensively kutetea hizo patched software, ama kweli katika hoja ambazo naziona ni very weak ni hii dhana ya kuhisi watu wanaotumia cracks hawana uwezo kifedha.
Huku ni kufikiri kizamani sana tena bila kushirikisha ubongo yaani mtu ambaye ameweza ku afford akanunua pc ya laki 5 ashindwe kununua CD ya antivirus ya 35 yenye 2 users?
Hapo umepwaya mzee kwasababu mimi sipendi kuwa limited kwenye bidhaa niliyoilipia wakati sehemu nyingine najua naweza pata full access ambayo niko huru (tena for free). Haiwezekani uniuzie godoro bei juu halafu uninyime usingizi
Mfano mimi sipendi iphone kulingana na limitation zake kwasababu kuna upande wa pili (android) hizo services ni free na huwekewi limit, sasa anakuja mtu kama wewe anasema sipendi iphone kwasababu sina gharama za kuimudu
Inawezekana kweli ni kawa sipendi iphone kwasababu sina gharama lakini sometimes sio kila anayetoa pesa bila mpangilio au kimahesabu ahesabike kama ni mkwasi, mda mwingine unaweza ukatoa pesa kwasababu hauna ujuzi wa kujua kua hicho unachokinunua kuna mahali kina patikana for free bila kujibana
Ebu icheki hii, nachukua 35k nanunua antivirus yenye 2 users tayari ishakuja na limit kwamba hata ikitokea nimepiga windows mara tatu basi sitaweza ku run hiyo antivirus tena. Wakati ukiwa na crack hauwi limited muda wowote utaojiskia kupiga window au kufanya mabadiliko yoyote haupati hiyo bugdha.
Bora hata ambao wanaosema cracks ni illegal kwasababu haina hati miliki na pia haimfaidishi official developer