Pamoja na utandawazi kuenea lakini bado kuna watu wananunua antivirus, windows, software za kwenye CD madukani

Smfh
 
Unapotumia software ambayo ipo Cracked that means hata zile official terms and security za software husika wewe hazikuhusu.. hata kama unaweza ona hupati virus Bado Kuna namna wanafaidika na wewe hasa kwenye kuiba taatifa zako pasipo wewe kujua.

Ndo maana ofisi za serikali huwa zinatumika software ambazo ni genuine.

Kutumia software ambazo ni cracked ni risky kama ni mtu ambae unapenda privacy.. unless ujue jinsi ya kujilinda kwenye taarifa za ulizo tunza kwenye kifaa husika.

Ni sawa na wale wanaotumia Gb What's up.. wanajionaga wameyapatia Sana maisha ila ukweli ni kwamba wao ndo wamepatikana vibaya mno..!!
 
Jamaa tuelekezane hilo chocho man hali za kiuchumi kwetu ni ngumu
 
Mkuu hii initial yako ya mwisho inanifurahisha balaa
 
Hoja ya umasikini inabaki palepale. Kunasoftwere zinauzwa m2 na hadi m4. Mfano pc nayotumia nina program moja ina gharimu 2m nyingine 1.2m nyingine dola 350. Hizo ni baadhi tu. Bila cracks hali ingekua ngumu. Umasikini shida
 
Uko sahihi
 
Wengine humu hata hiyo OS ya windows iko activated na KMS Autonet unless otherwise wawe wanaactivate kila baada ya miezi sita.
Ila kama mnabahatika kusoma zile Readme za crack huwa wanasema kuwa "support the developer if you use the software"
 
Software za kucrack siyo nzuri, mimi nikiwa na uwezo wa kununua software ambazo hazizidi 50 - 80$ nanunua tu, leo nimetoka kulipia software ya doodly 64$.
Asicho kijua mtoa mada ni kwamba unacho nunua kwenye CD sio software package bali ni activation keys hivyo unaweza ukaachana na package ya kwenye CD una download updated package halafu uka activate kwa hizo hizo keys

Software za wizi (cracked) sio nzuri kama unafanya kazi ya software kwa biashara.

Huwezi kumuwekea mteja wa kampuni,taasisi au shirika antvirus au operating system cracked utaaribu kazi ya watu.

Hizo wawekee watengeneza singeli wa mtaani huko kwenye pc zao na waingiza nyimbo kwenye memory huko ila sio kwa kampuni au taasisi au shirika ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…