Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Huu mradi una maswali mengi ambayo binafsi ninakosa majibu. Tunajua na kutambua kwamba kuna gharama za uendeshaji wa mradi, ikiwemo kulipa mishahara wafanyakazi,mafuta, matengenezo n.k Lakini biashara yoyote ambayo ina wateja wengi kiasi kile, Nilitegemea mpaka sasa biashara hii ingekuwa imekua hasa ukizingatia katika route za mwendokasi mfano kutoka Kimara mpaka Gerezani hakuna mpinzani kwasababu route zote za daladala zilifungiwa kupisha mwendokasi pekee kutoa huduma.
Swali fikirishi, inakuwaje biashara yenye wateja wengi kiasi kile tena isiyokuwa na mpinzani inaelekea kufa? Inakuwaje biashara yenye wateja wengi mno badala kukua na kuboresha huduma kwa kuongeza magari ndiyo kwanza inageuka kero na inaelekea kufa sasa? Viongozi wapo, wanashuhudia na hatuoni tamko/juhudi/hatua zinazoonekanazikichukuliwa?