Pamoja na yaliyo tokea lakini Simba atafuzu robo fainali kwa kuongoza kundi

Pamoja na yaliyo tokea lakini Simba atafuzu robo fainali kwa kuongoza kundi

Nyinyi pigeni tu hesabu zenu za kwenye makaratasi. Ila hatutaki tu kuzisikia tena zile kelele zenu za kuwakataa wachezaji, kocha na viongozi wa timu.
Hizo hesabu hazikupigwa kiholela, njia ya kwenda robo fainali tena kwa kuongoza kundi ni nyeupe sana, wakileta usenge tena lazima tupige kelele.
 
Yaani hawa watu wanachosha
Kuna mmoja alisema eti Asec kapata ngekewa kuongoza kundi
Nikamuuliza Kati ya Asec na Simba ambae hajashinda mechi yoyote ya CAFCC mpaka sasa Nani ana ngekewa?
Wanapiga hesabu utafikiri wanacheza pekee yao
Simba hata akilowana bado ni Simba usije ukamshika sharubu, Asec bora iliyokuwa na akina Azizi ki na Karim konate ilichapika 3-1 kwa mkapa na simba mbovu ya akina peter Banda. Mnyama anachukua point 3 Abidjan.
 
Mechi dhidi ya Wydad kwa Mkapa ndo mechi ngumu zaidi, sioni namna Simba itachukua point 3 siku hiyo.

Naiona droo au Simba kupoteza tena.
 
Mechi dhidi ya Wydad kwa Mkapa ndo mechi ngumu zaidi, sioni namna Simba itachukua point 3 siku hiyo.

Naiona droo au Simba kupoteza tena.
Mechi ngumu zaidi kwa simba ilikuwa jana na Wydad tuliwamudu vizuri tu tena kwao, siwaoni wakitoka kwa mkapa, mechi itakuwa ngumu sana kwa upande wao.
 
Mechi dhidi ya Wydad kwa Mkapa ndo mechi ngumu zaidi, sioni namna Simba itachukua point 3 siku hiyo.

Naiona droo au Simba kupoteza tena.
Mnyama ana asilimia zaidi ya 90 kushinda hivyo kaeji kwa kutulia.
 
kama mlitoa draw na asec kwa mkapa, sahauni kumfunga nyumbani kwake, pale mnaenda kupigwa nyingi, wydad na galaxy mkijitahidi mtatoa nao draw.

5IMBA GUVU MOYAAAA
Wydad ameshashinda jana, ni kama ameibua matumaini mapya ya kusonga hatua inayofuata, ili apate uhakika zaidi, ni lazima apate ushindi dhidi ya Simba kwa Mkapa.

Na hapo ndipo kipengele kilipo, hiyo game ni kila timu itacheza kufa na kupona, ni tough match kweli kweli.
 
Yaani Asec hana cha kupoteza??
Yaani eti kindezi tu amuache simba aongoze kundi??

Uwezo wa simba kwenye hilo kundi ni kumfunga Galaxy pekee kwa mkapa.

Simba atamaliza akiwa na point zisizozidi 6. Ni point 6 au chini ya hapo na si zaidi.
Mashabiki wa Simba sijui kama wanajua kwamba Wydad game ambayo itawapa uhakika hata wa 70% kufuzu hatua ya makundi kwenda robo ni dhidi ya Simba kwa Mkapa. Hiyo game itakuwa ni ngumu haswa kwa Simba.
 
Robo siyo stori tena kwa Simba..!! Yaani mkiishia robo, hilo ndo mliwezalo..!! Maana mmeshapiga robo nne mpaka sasa..!! Na ndani yake kuna robo ile ya uchawi, a.k.a tambiko hatarishi kule bondeni kwa Madiba. Na msipoangalia, mwakarobo itakuwa Mwakakundi mwaka huu
Lile tambiko lilikuwa hatari mkuu
 
Haya mjitokezee mechi yenu na Wydad Dar,ila mpira sio hesabu za matikiti,muheshimu mpinzani wako Galaxy alikuweka tatu kwa Mkapa.
Tena timu ilikuwa na vijana kuliko sasa walivyo wazee.
 
Habari wakuu

Wengi wenu mtakumbuka msimu uliopita nilifanya utabiri wa namna kundi la simba litakavyoisha baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo na ndivyo ilivyokuwa mwishoni, utabiri ulienda exactly kama ilivyo tarajiwa.


Hivyo nataka nifanye utabiri wa kundi la simba tena kwa msimu huu. Mpaka sasa Simba ana point 2, Wydad 3, Jwaneng 4, Asec 7. Asec achana nao kwakuwa wao tayari wamejipata.


Mechi ijayo simba atarudiana na Wydad hapa dar es salaam kwa vyovyote simba ahakikishe anamfunga wydad achukue point 3 ukijumlisha na zile mbili alizonazo zitakuwa 5, Asec atamfunga tena Jwaneng hivyo atafikisha point 10 huku Wydad atabaki na point zake 3.


Matchday 5 simba atacheza na Jwaneng Galaxy kwa mkapa na atachukua alama 3 hivyo atafikisha point 8, wakati huo huo Wydad atamfunga Asec na kufikisha point 6( sio guarantee anaweza kushangazwa vilevile na Asec ambapo itakuwa bora zaidi kwa simba).


Mechi ya mwisho Wydad atamfunga Jwaneng Galaxy na kufikisha point 9 huku akisubiria matokeo ya marudiano ya mechi ya Sinba dhidi ya Asec Mimosas ambao kwa point zao 10 tayari watakuwa wameshafuzu hivyo mechi kuwa rahisi kwa simba.


Uwezo wa kumfunga Asec nyumbani kwake simba anao na ukitazamia atakuwa tayari ameshafuzu hivyo hana cha kupoteza. Hivyo simba atachukua point 3 kwa Asec na kufikisha point 11, hivyo Simba atamaliza kwa kuongoza kundi akiwa na point 11, Asec nafasi ya pili na point 10, Wydad nafasi ya tatu na point 9, Jwaneng Galaxy nafasi ya mwisho na point 4.

Kwa wale ndugu zetu kwenye kundu lao watamaliza wa mwisho ila wakipambana sana wanaweza kumaliza nafasi ya 3.

Simba nguvu moja [emoji881]
Mechi five ni Asec vs Simba
Jwaneng vs Wydad
Mechi six ni Simba vs Jwaneng
Wydad vs Asec
 
Simba ataongoza kundi mkuu acha ubishi
Siyo rahisi na haitawezekana.
Mechi zimebaki tatu akishinda zote atakuwa na point 11 mpaka sasa anahitaji point 9 Asec anahitaji point 5 tu kwenye mechi tatu kuwa na 12 ambazo mwenye nafasi za kufikia ni Wydad Jwaneng na Asec pekee.

Hesabu anazopaswa kupiga Simba ni za kufuzu siyo kuongoza kundi
 
Siyo rahisi na haitawezekana.
Mechi zimebaki tatu akishinda zote atakuwa na point 11 mpaka sasa anahitaji point 9 Asec anahitaji point 5 tu kwenye mechi tatu kuwa na 12 ambazo mwenye nafasi za kufikia ni Wydad Jwaneng na Asec pekee.

Hesabu anazopaswa kupiga Simba ni za kufuzu siyo kuongoza kundi
Soma vizuri mkuu uelewe nilichomaanisha, Asec kwenye mechi zake 3 atashinda moja na kupigwa mbili.
 
Back
Top Bottom