Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
Panama wana machaguzi mawili tu kukubali ama kukataa na kila chaguzi lina matokeo yake hasi ama chanya.
Maoni ya mdau
Kabla ya raisi Trump kushika madaraka kwa mara ya pili aliweka wazi baadhi ya ndoto zake ikiwemo kuudhibiti mfrereji wa Panama unaounganisha bahari ya Pacifi na Atlantic.
Mara kadhaa raisi Trump ametoa kitisho cha kuuchukua kwa nguvu mfereji huo ambao waliujenga mwanzo mwa karne ya 20.
Hapo juzi katibu mkuu wa serikali ya Marekani Marco Rubio alienda Panama na baada ya kuondoka akatangaza kuwa kuanzia sasa meli za Marekani hazitalipa tena ada ya kutumia mfereji huo wenye urefu wa mali 51.
Raisi Mulino wa Panama ameshtushwa na tangazo hilo ambapo amesema Panama itaendelea kuwa na mahusiano na ushirika na Marekani lakini hawana mpango wa kuiondolea ada nchi hiyo na wala kuruhusu taifa hilo kuwa na mamlaka ya mwisho wa mfereji huo tena kwa njia za uongo na hadaa.