PANAMA machaguzi ni mawili tu ni akubali Panama Canal irudi chini ya usimamizi wa Marekani au avamiwe, Trump kazi kaanza

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Panama wana machaguzi mawili tu kukubali ama kukataa na kila chaguzi lina matokeo yake hasi ama chanya.

Panama.png

Panama 2 .png

Maoni ya mdau
Kabla ya raisi Trump kushika madaraka kwa mara ya pili aliweka wazi baadhi ya ndoto zake ikiwemo kuudhibiti mfrereji wa Panama unaounganisha bahari ya Pacifi na Atlantic.

Mara kadhaa raisi Trump ametoa kitisho cha kuuchukua kwa nguvu mfereji huo ambao waliujenga mwanzo mwa karne ya 20.

Hapo juzi katibu mkuu wa serikali ya Marekani Marco Rubio alienda Panama na baada ya kuondoka akatangaza kuwa kuanzia sasa meli za Marekani hazitalipa tena ada ya kutumia mfereji huo wenye urefu wa mali 51.

Raisi Mulino wa Panama ameshtushwa na tangazo hilo ambapo amesema Panama itaendelea kuwa na mahusiano na ushirika na Marekani lakini hawana mpango wa kuiondolea ada nchi hiyo na wala kuruhusu taifa hilo kuwa na mamlaka ya mwisho wa mfereji huo tena kwa njia za uongo na hadaa.

  • Thanks
Reactions: K11
Halafu Russia wakichukua Crimea watu wanabana pua, Israel akichukua Judea watu wanabana pua Tanganyika wakiichukua Zanzibar watu wanabana pua moroco wakichukua west sahara watu wana bana pua, iran akichukua kisiwa kile cha UAE watu wanabana pua. Hii dunia ni ubabe ubaben. Ndio maisha
 
Changamoto kila mahali hii dunia haitaki kujitilia huruma
 
Halafu Russia wakichukua Crimea watu wanabana pua, Israel akichukua Judea watu wanabana pua Tanganyika wakiichukua Zanzibar watu wanabana pua moroco wakichukua west sahara watu wana bana pua, iran akichukua kisiwa kile cha UAE watu wanabana pua. Hii dunia ni ubabe ubaben. Ndio maisha
Rwanda Akiipiga Congo Kupitia M23 Watu Wanabana Pua
 
Halafu Russia wakichukua Crimea watu wanabana pua, Israel akichukua Judea watu wanabana pua Tanganyika wakiichukua Zanzibar watu wanabana pua moroco wakichukua west sahara watu wana bana pua, iran akichukua kisiwa kile cha UAE watu wanabana pua. Hii dunia ni ubabe ubaben. Ndio maisha
China akichukua jimbo lake la Taiwan wanadai ni uvamizi
 
Trump alijibu hawezi jisumbua kuihakikishia usalama Taiwan wanapaswa wao kulipia gharama hiyo
Na leo kaipiga tarriffs canada na mexico kwa 25% na canada wamejibu pia.
Ulaya sijui kairoga. Kwa mambo yalivyo ni bora Ulaya ijiweke karibu na china kuliko Marekani maana hata wao hawajui nini kitawakuta. Ni bora wawahi watafte mbinu mbadala ikiwemo kuanza kutumia mifumo mpya ya malipo maana hakuna picha wataacha ona.
 
China akichukua jimbo lake la Taiwan wanadai ni uvamizi
Na hapo huwezi kusikia UN wanaongea. Ingekuwa nchi nyingine pale aliposema tu kuwa anataka kuinunua Greenland ila pia hajaweka pembeni uvamini wa kijeshi, hii kauli angeitoa China au Russia ulaya na marekani wangepiga kelele mpaka basi.
Korea kusini naye ajipange, na japan pia waanze kuwekeza kwenye silaha na ulinzi.
Ndani ya miaka 5 geopolitics and economy inabadilika kwa kasi ya 5G.
Kuna nchi kibao zitaanza kutafuta allies wengine hasa China maana kwa sasa Marekani si reliable tena.
 
Na leo kaipiga tarriffs canada na mexico kwa 25% na canada wamejibu pia.
Ulaya sijui kairoga. Kwa mambo yalivyo ni bora Ulaya ijiweke karibu na china kuliko Marekani maana hata wao hawajui nini kitawakuta. Ni bora wawahi watafte mbinu mbadala ikiwemo kuanza kutumia mifumo mpya ya malipo maana hakuna picha wataacha ona.
France imesema itawasaidia Denmark kuilinda Greenland dhidi ya U.S incase kikinuka anytime
 
Back
Top Bottom