Panapo majaliwa mwakani nitajiunga rasmi na siasa za nchi hii. Je, ungependa nifanye siasa na chama kipi?

πŸ˜€πŸ˜€
Kimambi sio mwanasiasa ni mwanaharakati.
Mimi nitawakomboa nikiwa kama mwanasiasa.

Naombeni ushirikiano, katika kazi Hii nzito.
Neno "komboa" linatumika vibaya.Mkombozi ni Mungu tu.Wengine washereheshaji maishani.Umkomboe mtu?Unamkomboaje?
 
Umekosea kuweka wazi mipango yako kama hii hadharani.
 
Ukombozi unahusu mkomboaji na mkombolewa. Wote wananufaika.
Hivyo neno hilo haliepukiki hapo.

Huwezi komboa kitu usichonufaika nacho😊😊
Tulia na utafakari kwa kina hilo neno.Ni sawa utueleze unataka utuokoe.Utaonekana kibweka tu.
 
Andiko murua kabisa ila ka nakuona mitaa ya lumumba vile
 
Tujadili Kwa Hoja Sasa,
Wewe ukiambiwa neno ukombozi na mkombozi nini kinakuja kwenye Akili yako?

Hapa tutajifunza wote
Kwa ufupi maneno mengi hutumika katika jamii bila mlinganyo wa maana.Tunayatumia kwa mazoea tuliyoyaanzisha au tuliyoyakuta.Neno kukomboa linajikita katika kumuondoa mtu na madhila makubwa au hali ya awali na kumpeleka pema.Neno hili linafaa na kupendeza kutumika kiimani zaidi kuliko kutumika kwa kupamba muendelezo wa kawaida wa maisha.Kumpa mtu mbinu za maisha hakufanani na ukombozi zaidi ya kumfundisha njia mbadala tu.Hata hivyo,sikuzuii "kuwakomboa bin kuwaokoa" watu wako.
 

Kwenye Lugha kuna kitu kinaitwa Visawe (Synonyms), yaani maneno tofauti kimatamshi na kimaandishi lakini yanayorejelea maana moja au maana inayokaribiana. Kwa mfano neno Pesa, Hela, mkwanja n.k.

Neno Ukombozi Kwa lugha ya kingereza hasa kwenyw Muktadha wa Siasa na utawala litatumika kama Liberation, ambapo litahusu kuwafanya Watu wawe huru kutoka kuwa wafungwa au watumwa na kuwapa Haki Sawa na nafasi Sawa katika kuyafanya Maisha Yao.

Katika Muktadha wa kidini, neno Ukombozi litatumika kama Redemption au Salvation. Ambapo litakuwa na maana ileile ya kuwapa Watu Uhuru lakini katika kipengele cha Nafsi au Roho.

Liberation, Redemption, Salvation ni Visawe vinavyorejelea maana ya kumuweka MTU huru, yaani kumtoa kwenye janga au tatizo au changamoto Fulani na kumfanya awe Huru.

Ukombozi unahusu fikra, Roho, mwili, na Hisia.
Pia upo ukombozi wa kijamii, kisiasa, kiutamaduni, ambao wote unategemea fikra, Roho, mwili na Hisia.

Kumpa mtu wazo, Elimu, ujuzi, maarifa, ufahamu, n.k. Utakuwa umekomboa MTU huyo kifikra, Kiakili, kimtazamo, kifalsafa ambayo mambo hayo ndio huleta mambo mengine.

Hujawahi sikia ukombozi wa Mwanamke ambao ulianza miaka ya hivi karibuni, na sasa umechanganya na Matokeo tunayaona?
 
πŸ˜€πŸ˜€
Kimambi sio mwanasiasa ni mwanaharakati.
Mimi nitawakomboa nikiwa kama mwanasiasa.

Naombeni ushirikiano, katika kazi Hii nzito.
Hamna cha ukombozi we nunua mashati ya kijani, vitenge vya kijani shona mashati, sifia sifia jikombe kombe pata nafasi jaza tumbo lako inaisha hivo......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…