Fernando Wolle
JF-Expert Member
- Aug 19, 2022
- 387
- 770
Kuna shughuli na kazi za kila siku tunazozifanya kujipatia mahitaji yetu muhimu na kujenga uchumi wetu Binafsi, na kuna kazi zinazoweza kukupa sifa mbele za watu lakini hazitakupa hatma nzuri yenye tija ya uchumi toshelezi wa maisha yako.
Kibaya zaidi kazi za namna hiyo zinachukua muda mwingi sana kuliko chochote unachofanya kwa siku. Fikiria kwa umakini, tafakari na pima kama kazi hiyo inayokuchukua masaa zaidi ya 9 kwa siku Je, inakupeleka wapi? Je, unaona utakuwa wapi baada ya Mwaka mmoja, miwili, au mitatu?
Kama unaona hakuna future ya hiyo kazi, achana nayo hata kama inakukalisha kwenye kiyoyozi na kukupa sifa kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Angalizo, usiiache hiyo kazi kama huna sehemu ya kukupa hatma nzuri ya baadae. Lakini kumbuka tu kwamba kile kinachokula muda wako mwingi kwa siku ndicho kilichobeba na kitaamua hatma yako.
NAWASILISHA.