Pande mbili: Yaani Serikali na CHADEMA, vitafakari Kwa makini, athari zitazotokea, iwapo maandamano hayo yaliyoandaliwa na CHADEMA yatafanyika

Eh kumbe maandamano yameandaliwa na Chadema, nikajua yameandaliwa na wananchi.

Hakuna maandamano ya kuipinga serikali yanayoanzishwa na chama pinzani yakafanikiwa.
Haswaa ingekuwa ya wananchi hata mm yangenihusu ila ya chadema acha wapigwee tu
 
Kwa hiyo niwasihi wana-CHADEMA nao walizingatie Hilo Kwa umakini mkubwa.
Sijui ulicho andika katika bandiko lako hilo refu; lakini nikiangalia kichwa cha mada na mstari huo wa mwisho naona kama ni mizunguko tu mirefu isiyokuwa na maana yoyote.
Mwenye wajibu ni serikali kuzuia maandamano kwa kuwa wawazi juu ya utekaji na kuuawa watu.
Watoke mbele wawaeleze wananchi kwamba vitendo hivyo siyo vya kiTanzania na kwamba taarifa zote zilizopo kuhusiana na mambo hayo wanawaeleza wananchi waziwazi.
Sasa sijui unawa shauri kitu gani CHADEMA na waTanzania wengine kuhusu ushiriki wa serikali katika kutafuta ufumbuzi wa jambo hili.
 
Rejea
Katiba yetu ibara ya 20 imetoa haki ya kukusanyika sio tu kwa amani bali mikusanyiko hyo iwe kisheria.
Sheria ya vyama vya siasa ,sheria ya polisi na polisi wasaidizi S43 imeelekeza wazi utaratibu wa kufuata kabla ya kukusanyika kihalali.
Lakini pia kanuni ya adhabu S.74-83 imetoa tafsiri ya mikusanyiko isiyo halali na adhabu zake.
Kama unadhani CDM wanahaki kisheria ya kukusanyika na kuandamana kwa hiyo mihemko ya mitandaoni tukutane hiyo 23 dola itahakikisha mtu amechakaa na kufubaa
 
Damu ikimwagika ipo mikononi mwa mbowe!
 
..tatizo letu ni kujiaminisha kwamba maandamano ya wapinzani yakifanyika, response ya Polisi lazima itakuwa kuumiza, na kuuwa waandamanaji. Ni sawa na kuaminini kwamba wapinzani wanastahili kuumizwa au kuuwawa na Polisi. Wapinzani wakiumizwa au kuuwawa jamii haipati mshtuko unaostahili pale binadamu anapouwawa.
 
Positive and negative impact
 
Mkuu tuwe makin TUTAPIGWA SANAAA 23.9.2024
 
Kipindi hiki kinachoendea uchaguzi huwa ni kipindi kigumu sana kwa vyama vya upinzani vyenye nguvu. Mimi niwashauri CDM, mda huu watapata Maumivu mengi na hasara kubwa sana kama watajiingiza kwenye Maandamano au mvutano na POLISI. Hivi Sasa humu nchini kuna vyama vikuu viwili tu vya siasa ambaavyo vinagombana ni CDM na Dola, CCM kimekaa pembeni kimya kikisubiri mda tu wakukabidhiwa ushindi wao wa Mezani. Mimi nishauri CDM wasitumie nguvu nyingi mda huu kwani chama wanacho shindana nacho ambacho ni Dola kina silaa wao bado hawana hata fimbo wataumia, Chakufanya wawe wapole waendelee kuhamasisha wananchi waendelee kujiandikisha wakichokozwa wasijibu mapigo nguvu zote wazielekeze kwenye uchaguzi. Wajitahidi kuwalinda wanachama wao na watia nia wao wauchaguzi waserilkali za mtaa. Uchaguzi hautakuwa Raisi kwani mgimbea mwenzao anabunduki wajiandae kisaikolojia vhochote kinaweza tokea kama Rais alivyo waambia Jeshi la wananchi. Wakiona Mbungi nzito waachie wananchi waamue wenyewe. Wasihamasishe chochote, kwani hii nchi ikipasuka hakuna mtu atakuwa salama.
 
Umesema katiba yetu imetoa haki ya makusanyiko/maandamano ya amani.

Kwamba utaratibu unapaswa kufuatwa (utaratibu unaoelekezwa na katiba ni pamoja na kutoa taarifa/zingatia neno kutoa taarifa juu ya uwepo wa maandamano)

je, unawezaje kusema chadema hawana haki ya kufanya maandamano yao ikiwa sheria inawaruhusu kufanya hivyo ?

unavyosema “dola itaacha mtu kachaka na kufubaa,,. je, kazi ya dola ni kulinda usalama wa raia na mali zao pindi maandamano yanapo fanyika au kazi yao ni kuchakaza waandamanaji walio jitanabaisha kupaza sauti zao kwa amani?

Au wewe ni kada unaefurahishwa na maovu yanayoendelea ikiwepo kutekwa na kuuwawa kwa watanzania wenzetu?
 
Kuna vijana wajinga sana wanatumika kutisha na kutukana humu bila hata hoja
 
Kwani polisi wakiwalinda waandamanaji wakaandamana kwa amani kuna shida gani?
 
Watu wanaandamana bila silaha yoyote wala fujo yoyote na ni kwa mujibu wa Sheria na Katiba kuna tatizo gani hapo ndugu zangu. Au basi walioshindwa kuzuia mauaji ya wananchi wajiuzulu kama uungwana wa kujutia hali iliyotokea hapo napo kuna shida gani ndugu zangu. Mungu mbarike Rais wetu na Mungu ibariki Tanzania.
 
..Chadema wamesisitiza maandamano ni ya amani.

..Kama Polisi wana taarifa za mtu / kikundi kinachotaka kufanya vurugu basi wawakamate hao, na sio kuzuia maandamano yote.
Maandamano ni halali kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Rejea Ibara ya 20 ya Katiba ya mwaka 1977. Rejea pia kifungu cha 11 (4) na (5) cha sheria ya vyama vya siasa.
Kimsingi watu wana haki ya kukusanyika pamoja, kutoa maoni na kuandamana.

Huo ndo msingi wa Sheria na utawala Bora kwenye Katiba na Sheria zetu!
Haya masuala ya Malkia au machawa kutaka matakwa yao ndo yawe Sheria ni kinyume kabisa na misingi iliyopo!

Polisi wao wajibu wao ni kupokea Taarifa ya mikusanyiko au maandamano kutoka kwa waratibu kisha watoe sababu zenye mantiki kuridhia ama kukataa. Uamuzi ambao pia unaweza kupingwa mahakamani!

Kupiga marufuku maandamano kwa sababu zozote za kumlinda Malkia na machawa wake ni kukandamiza haki za raia!

Kama bibi yake Lucas Mwashambwa na jingalao wanaupiga mwingi kwanini polisi watumike kupiga marufuku maandamano ya amani?

Mtayapiga marufuku Hadi lini? Au mnataka wasiwe wanawapa taarifa yenye kusudio la kuandamana?
 
Kitendo cha cdm kuogopa kuandamana ni kurusu kuendelea kufanyiwa unyama na vyombo vya dola kwa faida ya ccm. No gain without pain. Bila mauaji cdm wasitegemee mabadiliko yoyote.
 
Hayo maandamano wanataka wafanye wao tu... yaani ni ruksa wao waandamane nchi nzima kumpongeza Malkia chura kiziwi. Na si vinginevyo!

Ila Wewe subiri.... Siku zaja ambapo maandamano ya kuwapinga yataibuka ghafla kila pembe ya nchi!

It is just a matter of time. Tanzania si kisiwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…