Pande mbili: Yaani Serikali na CHADEMA, vitafakari Kwa makini, athari zitazotokea, iwapo maandamano hayo yaliyoandaliwa na CHADEMA yatafanyika

Kitendo cha cdm kuogopa kuandamana ni kurusu kuendelea kufanyiwa unyama na vyombo vya dola kwa faida ya ccm. No gain without pain. Bila mauaji cdm wasitegemee mabadiliko yoyote.
CDM wakizuiliwa kuandamana kama bado Wana ustaarabu waende mahakamani kupata tafsiri ya Kisheria.

Wasikubali. Wasirudi nyuma! Walete vurugu na wauaji ni wale wenye bunduki!
 
Hadi sasa inaelekea Kuna mvutano mkubwa Kati ya serikali na CHADEMA, kuhusu maandamano ya amani, yaliyopangwa na CHADEMA tarehe 23 mwezi huu, kama serikali itakuwa haijatoa taarifa yoyote kuhusu kifo Cha kiongozi wao Ali Kibao na haitaeleza walipo viongozi wao wa vijana, akina Deusdedit Soka na wenzake wawili, ifikapo tarehe 21 mwezi huu.

Kwa hali ninayoiona kutokana na hotuba iliyotolewa na Rais Samia, katika sherehe za kuadhimisha miaka 60, tangu Jeshi hilo lianzishwe, dalili ni finyu sana kufikiwa muafaka wa suala Hilo.

Rais Samia alitoa msimamo wa serikali yake kuwa, haiwezi kuelekezwa Cha kufanya na mabalozi wa nchi za nje, viongozi wa vyama vya upinzani hapa nchini na viongozi mbalimbali wa dini, walioiomba serikali, iunde Tume huru ya kuchunguza Kwa visa hivyo vya kutekana na baadhi ya wahanga hao kuuliwa.

Ingawa Kila upande unavutia upande wake, Kwa upande wa serikali, ukionya vikali kuwa maandamano hayo imeyapiga marufuku, wakati chama Cha CHADEMA kikidai kuwa maandamano hayo yapo pale pale, kama yaliyopangwa, Kwa sababu serikali haijatoa majibu Kwa masuala iliyoyauliza.

Ni wazi kuwa kutokana na mtifuano huo mkali, nchi yetu ipo njia panda ya kuelekea Kwenye machafuko ya umwagikaji wa damu, iwapo CHADEMA watatekeleza kuingia Kwenye maandamano hayo kama walivyopanga.

Nianze Kwa upande wa serikali, ni lazima itafakari Kwa makini kuyapiga marufuku maandamano hayo ya amani yaliyoratibiwa na CHADEMA, kuhusu athari itakazozipata iwapo itatekeleza azma yao ya kuyavunja maandamano hayo, hata kama ni Kwa kutumia nguvu.

Kwanza, ni jambo inalosikitisha na linaloonyesha wazi kuwa serikali hii, imepuuza, madai yote ya CHADEMA, Jumuia ya Kimataifa, viongozi wakuu wa dini mbalimbali, pomoja na wanaharakati mbalimbali, waliotaka serikali iunde Tume huru ya uchunguzi, Ili ibainike wahusika wa vitendo hivyo viovu.

Ifahamike pia kuwa Jumuia ya kimataifa itakuwa macho, kuangalia matokeo ya maandamano hayo, Kwa kuwa na wao ni miongoni waliotoa wito Kwa serikali hii Ili iunde Tume huru ya uchunguzi.

Kwa maana hiyo, iwapo maafa yatatokea Kwenye maandamano hayo, watatoa ripoti Kwenye nchi zao na hivyo picha ya nchi yetu kimataifa, itakuwa imeharibika mno na ipo hatari, misaada na mikopo mbalimbali ambayo nchi yetu imekuwa ikipata kutoka Kwenye nchi hizo, itakuwa ndiyo mwisho wa kuipata!

Nije Kwa upande wa CHADEMA, ingawa wao Wana haki zote za kuandaa maandamano hayo ya amani, kutokana na wao kuona kuwa hawatendewi haki na hata Katiba ya nchi yetu inaruhusu kifanyika Kwa maandamano hayo na njia pekee, wanayoona wao iliyosalia ni kufanya maandamano hayo ya amani.

Hata hivyo naomba pia kuwatahafharisha CHADEMA kuwa na wao wanapaswa kutafakari Kwa makini, kama maandamano hayo yafanyike au laa, Kwa kuwa serikali hii imeshatangaza kibabe bila kutumia sheria yoyote ya kuyafuta maandamano hayo, sasa ukizingatia kuwa askari hao watakuja Kwa nia ya kupambana na waandamaji hao, ni dhahiri maafa yanaweza kutokea.

Kwa hiyo niwasihi wana-CHADEMA nao walizingatie Hilo Kwa umakini mkubwa.

Mungu ibariki Tanzania
Demokrasi Tanzania inazidi kuzama safari hii kinara wa yote haya ni Mama Samia.
 
Acha uoga wa kishamba , maandamano ni ya amani ,hamna kitakachoharibika ,hiyo nguvu inayotumia kudoubt maandamano ingetumia kuwaponda serikali na vikosi vyao vya mauaji dhidi ya wanachadema .
Chadema wanatimiza haki yao ya kikatiba
 
Umesema katiba yetu imetoa haki ya makusanyiko/maandamano ya amani.

Kwamba utaratibu unapaswa kufuatwa (utaratibu unaoelekezwa na katiba ni pamoja na kutoa taarifa/zingatia neno kutoa taarifa juu ya uwepo wa maandamano)

je, unawezaje kusema chadema hawana haki ya kufanya maandamano yao ikiwa sheria inawaruhusu kufanya hivyo ?

unavyosema “dola itaacha mtu kachaka na kufubaa,,. je, kazi ya dola ni kulinda usalama wa raia na mali zao pindi maandamano yanapo fanyika au kazi yao ni kuchakaza waandamanaji walio jitanabaisha kupaza sauti zao kwa amani?

Au wewe ni kada unaefurahishwa na maovu yanayoendelea ikiwepo kutekwa na kuuwawa kwa watanzania wenzetu?
Hayupo mtanzania mwenye akili timamu anayefurahishwa na kutekwa na kupotea kwa ndugu zetu
Vyombo vya ulinzi na usalama vimetoa tahadhari na kupiga marufuku kufanyika kwa maandamano hayo kwani taarifa za kiintelijensia zinaonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani.
Kupitia katazo na zuio hilo nilitegemea utii wa sheria pasipo kushurutishwa lakni isivyo kawaida bado wanang’ang’ania na kuendelea kuhamasisha maandamano hayo je huon ni dhahiri kua kuna lengo baya mbeleni?
Lakini ikumbukwe uchunguzi mzito unaendelea kufanyika juu ya tukio hilo na kwa taarifa zisizo rasmi inaonekana ni inside job . kuhamasisha maandamano n njia moja wapo ya kutoa wapelelez kwenye focus na kuamsha hisia tofauti
Kwa upeo wangu ingekua ni busara kama report ingetoka ya uchunguzi ndipo waipinge Lakin wanashinikiza vitu vifanyike underpressure .
Tukubaliane kua ni jukumu letu kulinda amani tuliyonayo kwa nguvu zetu zote. Tuendelee kuviamini na kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama
 
Back
Top Bottom