Umejibu kipengere kimoja tu. Hujaweka vigezo vyovyote ulivyotumia kuhitimisha maoni yako. Uongozi pia ni contingency ( unategemea mahali, aina ya watu unaowaongoza na wakati) Baraza la wawakilishi na Bunge la Jamhuri wa Tanzania) ni vitu viwili tofauti kwa maana ya watu na changamoto zake. Nikisikiliza mijadala ya Baraza la wawakilishi nikalinganisha na ile ya Bunge la Jamhuri ni kama naota ndoto. Linawafaa wenyewe. Hoja nyepesi mno na ndiyo maana hata mtu mwenye Diploma analiweza. Waliposema wanataka kutunga Katiba yao, hakuna aliyeweza kuona kama wanavunja Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Leo baada kuvunja ndipo wanaona maana ya kuwa na bendera wimbo wao waTaifa kuwa kumbe ilikuwa ni kuvunja Muungano. Kiongozi wa Baraza la wawakilishi ni huyohuyo unayemwita mwenye Hekima. Hekima maana yake ni kutatua migogoro bila ya kuleta athari zaidi kama Mfalme Seleiman wa kwenye Biblia. Alitatua tatizo la wanawake wawili waliokuwa wakigombea mtoto bila ya kupoteza uhai wa mtotowala kuumiza yeyote baina ya wanawake hasimu