JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Inadaiwa kuwa uongozi wa Klabu ya Simba un mipango ya kupitisha panga kwa wachezaji wao walioonyesha kushuka kiwango mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Hilo limeshapangwa lakini kwa sasa wameweka wazi kuwa mawazo yao yote yapo katika kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali wanayoshiriki ikiwemo ligi kuu ambayo wanapambana na Yanga.
Hivyo suala la kuwaongezea mikataba mastaa wao wanaomaliza mikataba litapatiwa majibu mwishoni mwa msimu
Baadhi ya nyota wa Simba ambao wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu na wapo kwenye htari ya kutoongeewa mikataba mipya ni Bernard Morrison, Taddeo Lwanga, Meddie Kagere, Chis Mugalu na Pascal Wawa.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema:
“Ni kweli kuna kundi kubwa la wachezaji wetu ambao wanatarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, hatujaanza mazungumzo nao lakini niwatoe hofu Wanasimba kuwa tunajua nini tunapaswa kufanya juu ya hilo na tutahakikisha wachezaji wote tunaowahitaji kwa msimu ujao wanapewa mikataba mipya.”
Chanzo: Global Publishers