Uko sahihi mkuu, Urusi inatakiwa iwe inachuana na Marekani kwenye kila nyanja muhimu ikiwemo kiuchumi ili kuweka mizani sawa,asiwepo mwenye nguvu mmoja.
Ila cha ajabu wamepokonywa hiyo nafasi na China, ila kwenye kutumia rasilimali zao vizuri wamejitahidi sana maana wamezua sana gesi huko Ulaya magharibi na imewatajirisha sana.
Kaka sio natetea tu Urusi,Urusi ilikua Bora Sana kiuchumi enzi za USSR,ikavurugika ikavunjikavunjika,zikatoka nchi nyingine mpya kabisa na Zina uchumi wao,Estonia,Latvia,Georgia,Lithuania,Khazakistan,Tajikistan,Azebaija ,Moldova,Ukraine,Uzebakista n,Berarusi n.k.
Sasa fikiria zote hizo zilikua majimbo ndani ya USSR.
Baada ya kuvunjika Urusi imekaa miaka kumi tu ikijijenga upya.China na USA zikiinjoi mshikamano wa majimbo yao.
Hivyo happy ilipo Urusi Sasa hivi inastahili sifa.
Zingatia inavyobaguliwa na kuwekewa vikwazo na west.Ni lazima ichomoze taratibu.
Fikiria ulikua bingwa wa riadha za masafa marefu duniani,katikati ya mashindano ukaanguka chini ukavunjika mguu,ukainuka,ukakaa hospitality miaka miwili,ukapona,ukarudi mashindanoni,ukashika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa wawili wa wakati huu.
Kwa kifupi Mimi ntakuona wewe Ni shujaa. hayo ndio mapito ya Urusi ya Putin.