Panya ana ajira, Kijana hana — na anasafiri kwa ndege!

Panya ana ajira, Kijana hana — na anasafiri kwa ndege!

Jamani jamani… dunia hii kweli ni kitendawili kigumu!

Leo tena nimerudi na habari mpya — panya mmoja anaitwa Ronin, si tu ana ajira ya kudumu ya kutegua mabomu, bali tayari ameshapanda ndege, amesafirishwa kwa heshima mpaka Cambodia!

Wewe kijana, umesoma mpaka ukakariri chati za periodic table, umefaulu mpaka ukaaminika kuwa tegemeo la familia,

lakini passport huna, na hata ndege ya Fastjet hujawahi igusa!

Lakini Ronin — panya wa kawaida mwenye mashavu makubwa — amepakiwa vizuri kwenye crate ya heshima,
akapanda ndege kimya kimya, akaenda kutumikia taifa la mbali!

Alifika kule anakaribishwa kwa mikono miwili, ana mafunzo ya kipekee, ana chakula maalum — na kazi yake? Kutegua mabomu kwa harufu tu.

Hebu tujiulize kwa uchungu mchanganyiko wa mshangaa

Ronin hajui hata kusoma "boarding pass" — lakini yuko Cambodia kwa ajira maalum.

Wewe CV yako imepigwa pini ya mshono, ila bado inalala kwenye email ya HR.

Ronin hana CV, hana referee, lakini ana kazi yenye heshima na exposure ya kimataifa.

Tunafeli wapi sasa?

Je, ni wakati wa:

Kujifunza kugundua mabomu kwa harufu?

Au kuanzisha harakati mpya: "Kampeni ya Vijana Kupata Ajira Kabla ya Panya"?


Mimi nauliza tu kwa niaba ya vijana wote wa taifa hili…

Ama kweli, duniani kuna mambo — na mengine yanapaswa kupigiwa magoti.

Uzi huu ni satire Wala Hauna maana iliyokusudiwa.
Usimwonee gere huyo panya. Wale Waajiri i.e. Cambodia ndo waliomtaka huyo. Wewe kijana endelea kujishughulisha; iko siku na wewe utahitajika mahali fulani. Endelea kupambana. Huyo panya halipwi "mshahara" bali malipo ni in kind na kidogo kwa boss wake.
 
Back
Top Bottom