Panya Magawa mahiri kwa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini amekufa nchini Cambodia

Panya wa kiume kutoka Tanzania, Magawa ambaye mwaka 2020 alitunukiwa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini nchini Cambodia, amekufa akiwa ni panya Mzee mwenye umri wa miaka minane ambao ni umri mkubwa kwa panya.

Mwezi November mwaka jana Magawa alitimiza umri wa miaka minane na alistaafu pia mwaka jana kutokana na uzee wake kwakuwa alianza kupunguza kasi ya kutegua mabomu.

Magawa alizaliwa Tanzania November 5,2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70 na hadi anakufa amenusa mabomu na silaha nyingine zaidi ya 100.

Magawa amefia nchini Cambodia kwakuwa baada ya kustaafu hakurejeshwa Tanzania na amekufa usiku wa kuamkia Jumapili ya juzi.
Kwa nini baada ya kustaafu hakurudishwa nyumbani? Cambodia watoe maelezo na warudishe maiti na mafao yake TANZANIA akazikwe kwao SUA
 
Panya Magawa ni panya ambae alizaliwa mkoani Morogoro Nchini Tanzania Mnamo 5 November 2014 akiwa na uzani wa kilogramu 1.2 urefu sentimita 70.
Kwa kabila Panya Magawa ni halfcast wa Kiluguru na Kipogoro

Panya Magawa alifariki mnamo akiwa na umri wa Miaka 8 na kuzikwa Nchini Cambondia, pia Magawa alistaafu kazi ya uteguaji mabomu na kugundua silaha mnamo mwaka jana yaani Mwaka 2021.
Magawa mnamo mwaka 2020 alitunukiwa nishani ya dhahabu nchini Cambondia.

Pia Magawa Alisoma shule ya awali mpaka chuo kwa miezi 10.
Aligundua zaidi ya mabomu 100 yaliyo tegwa.
Ameishi akiwa bachela.

Jina Magawa alipewa na mkufunzi wake Pendo Msegu ambae ni mkufunzi wa panya wengi katika chuo cha Sokoine university of Agriculture (SUA)
 
Duu, urefu wa 70cm , karibia mita 1
 
Back
Top Bottom