Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Wakati wa utawala wa Awamu ya Tano tulishuhudia kupungua kwa wimbi la uhalifu nchini lakini pia tuliona ongezeko la vijana kwenye sekta ya ujasiriamali na shughuli halali za kujiingizia kipato.
Baada ya kuanza kwa Awamu ya Sita, kipaumbele cha kwanza kilikuwa ni kuwazuia na kuwaondoa wajasiriamali na wachuuzi wadogo kutoka maeneo waliyokuwepo huku kukikosekana juhudi za kujenga ama kukamilisha masoko au maeneo ya masoko rasmi. Pamoja na uondoaji wafanyabiashara, serikali kupitia Halmashauri haikuzingatia upatikanaji wa mitaji kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu bali ilionekana wazi kuliundwa vikundi hewa na pesa ya umma ikawa imepotea namna hiyo.
Kama haitoshi,
Serikali imekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu hatima ya watoto wanaofeli mitihani ya darasa la Saba na Kidato cha nne bapo jeshi hilo huoshia mitaani, vijiweni na magenge ya uhalifu. Serikali inasisitiza malezi ya vijana kwenye familia lakini serikali hiyo hiyo inaweka ugumu kwenye uhakika wa
Ajira
Elimu
Malazi
Fursa
Usawa
Ustawi wa Jamii
Vijana wengi wakajiingiza kwenye shughuli za bodaboda ambapo imesaidia kwa kiwango kikubwa sekta ya usafiri maeneo mengi. Lakini serikali yetu mpaka leo haijaweza kurasimisha kisera biashara ya usafiri wa boda boda. Ingeweza kuwatungia sheria na taratibu za kufuata.
Leo tunajadili uhalifu wa vikundi vya Panyaroad ambapo vilishaanza kuwa historia yaani vilishafutika naturally. Kiongozi ambaye hajali huwa anawaona wale anaowaongoza ni kero kwake na hivyo hutumia mabavu badala ya kuweka mikakati ya kuzuia vijana kujiingiza kwenye makundi ama mwenendo wa uhalifu
Tangu jamii ilipojihalalishia maamuzi ya kuwaua wezi na vibaka, lakini vibaka na wezi hawajawahi kuisha kwenye jamii.
CCM imejaliwa kuwa na sera nzuri lakini imekuwa ni kichaka cha viongozi wasio na hekima