Panya road waibua taharuki Mbagala

Panya road waibua taharuki Mbagala

baada ya kujiona wote waoga unamlaum askari kama ninyi kundi mnakimbia yeye mmoja na efd mashine atafanya nini mnatia aibu sana..utadhani panya road ndio wanaume wengine woote wanawake acheni upuuzi huo..,
 
Kulikuwa na uwiano gani kati ya WANAUME WA DAR waliokimbia na panya road?
 
Tukio hili limetokea leo saa 3:usiku Mbagala mwisho na shuhuda wa tukio hilo nikiwa mimi mwenyewe, Nikiwa njiani narudi nyumbani kulitokea taharuki kubwa baada ya tetesi kusikika kuwa Vijana watukutu maarufu kama PANYA ROAD wamevamia stand ya mbagala wakifanya wakipora mali na kupiga watu hovyo ndipo wananchi walianza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao.
KILICHONISHANGAZA
Nikiwa kwenye foleni nimeshuhudia Trafiki waliokuwa zamu wakitimka mbio huku wakivua kofia na mashati yao meupe na kubaki na nguo za ndani maarufu kama sing'lendi.
Swali nalojiuliza hawa askari wetu wanashindwa hata kufanya upepelezi wa mwanzo kujua adui yuko upande gani,ana siraha gani na atakabiliana naye vipi.

Mkitaka tu hao Panya Road ' watokomezwe ' kabisa huko kwenu Mbagala jifanyeni kuwa mnataka kuandamana kupinga kununuliwa kwa Bombardier Q400 kisha semeni kuwa maandamano yenu mtayafanya tarehe fulani kutoka Mbagala kuelekea Plot namba 1 Opposite na Wizara ya Elimu kisha mtaona tu kuanzia hiyo siku mtakayotangaza hadi kuelekea siku yenyewe Vikosi vingi sana vya Ulinzi na Usalama vitakuwa vinapita kila mara huko kwenu huku vikifanya ' mazoezi ' ya hapa na pale na angani mtaona Ndege zinapaa kila sekunde huku Mitaani mwenu mtakutana na ' Mandata ' wakifanya Oparesheni ' maalum ' na hapa hao ' Panya Road ' wenu huko watakuwa ni ' Historia '. Huu ni ushauri wa bure Kazi kwenu.
 
Nina waiwasi hii panya road sasa inatumika kisiasa.Watu wakitaka kutusahaulisha mambo basi mambo madogo yanakuzwa na kupewa promo kuubwa ili kuyazika mambo makubwa.
 
Askari ana anafundishwa jinsi ya kupambana na adui mwenye siraha tatizoaskari wetu wali nazi.

Poa bob ila pia wanafundishwa ku take cover mpaka uwe na uhakika wa nguvu ya adui!!!
 
Ajabu ni watu wanaowacheka hao Askari na watu waliokimbia mana hao madogo huwa wanakuwa na vipande vya Nondo,nyembe,Koreo,Msumeno(wanaweka mfuko wa koti yale unayoyaona wakivaa majambazi kwenye muvi),bisibisi,maji ya betri na misumari ya inchi 6...sasa wewe upo mikono mitupu mazowezi yenyewe unafanya ya kukimbia usipogugeuza bucha mana kabla hawajaingia barabarani kukaba huwa wanavuta bangi huku wanalia na kunuizia maneno ya kiuaji tu
 
Tukio hili limetokea leo saa 3:usiku Mbagala mwisho na shuhuda wa tukio hilo nikiwa mimi mwenyewe, Nikiwa njiani narudi nyumbani kulitokea taharuki kubwa baada ya tetesi kusikika kuwa Vijana watukutu maarufu kama PANYA ROAD wamevamia stand ya mbagala wakifanya wakipora mali na kupiga watu hovyo ndipo wananchi walianza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao.
KILICHONISHANGAZA
Nikiwa kwenye foleni nimeshuhudia Trafiki waliokuwa zamu wakitimka mbio huku wakivua kofia na mashati yao meupe na kubaki na nguo za ndani maarufu kama sing'lendi.
Swali nalojiuliza hawa askari wetu wanashindwa hata kufanya upepelezi wa mwanzo kujua adui yuko upande gani,ana siraha gani na atakabiliana naye vipi.
HAO PANYA BUKU WANA NN ? MBONA WANAUME WA DAR (TRAFIK) MNAKIMBIA WATOTO WENU ?
 
Mh traffic hana silaha yeyote apambane na wajinga wasio na akili wenye mapanga...mbona mnataka tu kutusi askari wetu aisee
Kwa kweli

Hata mie ningekuwa traffic ningetiririka tu

Imagine huna silaha halafu upambane na kundi kubwa la waporaji wenye silaha za jadi za kutosha...as if kuna duka linauza uhai
 
Kwa kweli

Hata mie ningekuwa traffic ningetiririka tu

Imagine huna silaha halafu upambane na kundi kubwa la waporaji wenye silaha za jadi za kutosha...as if kuna duka linauza uhai
Hii ishu inataka kuifight kwa umoja na sio vinginevyo. Ndo maana FFU wako active saana maana huwezi kukuta askari wa FFU anafanya kazi mwenyewe...hapana!

Wanakuja kama unit wakiwa na ramani yao ya vita, wanajua wanaenda wapi na kumshughulikia nani..naamini FFU wakitumiwa vizuri wanaweza kunetraulize haya makundi in a matter of second sema ndo hivyo hawatumiwi ipasavyo, ndo maana hawa madogo wanatamba.
 
wanaume was dar acheni hizo mungu anawaona mlisimamia jamaa akatobolewa macho Leo mnasimamia vijitoto vinatishia stendi nzima ata mungu hapendi
 
Polisi wetu bhana.wako hoi.ingekuwa Islamic state sijui ingekuwaje
 
Nikijaribu kufanya comparison kati ya Dsm na baadhi ya mikoa,ukwel ni kwamba DAR hakuna usalama hata kidogo,ila kuna kelele za usalama tu.Mkoa ambao umepewa priorities na vifaa vingi kwa polisi na umegawanywa kwa kila hali kurahisisha utendaji wa polisi,ila hakuna usalama.Hao panya road hawajawah kufanya vurumai saa 8 usiku,huwa wanafanya mchana mwisho saa 3 usiku watu wakiwa machooo
 
Hakuna uhai mara mbili

Hapo labda hawana silaha yoyote zaidi ya efd mashine..... wacha watiririke tu.....
Ilaa hana hata namba ya simu ya kituo cha polisi awaite wenzie waje wawashuhudie?
 
Khaaaa,, hii aibu kweli kama askari wenyewe wanakimbia,,, loooohhh.., raia wa kawaida lazima watakuwa wanang'ang'ania kuingia uvunguni mwa kitanda..

Kwa hiyo wanaume wa dar bado wote wanaogopa panya road...🙁🙁
***
askari 2 labda kwa vijana 200, wat should he do?
#Ni-mbio tu.....
 
Back
Top Bottom