Panya road waibua taharuki Mbagala

Panya road waibua taharuki Mbagala

Nina waiwasi hii panya road sasa inatumika kisiasa.Watu wakitaka kutusahaulisha mambo basi mambo madogo yanakuzwa na kupewa promo kuubwa ili kuyazika mambo makubwa.
Haya mambo yapo....kuna mtu namfahamu mwezi tena mwanamama mjeda kavamiwa na panya road wanamtaka atoe hela na hakuwa nazo zaidi ya 40000 tu...wakazichuka na redio na wakamchana na panga mkononi..walibananisha mtaa mzima..usiku si chini ya 20 vitoto vidogo
 
Hapo stendi hapakuwepo na wanaume?

Hivyo vitoto vitavamiaje stendi na kuanza kupiga na kupora watu?

Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Yaani watu mpo stendi mnaachia vitoto viwapore na kuwapiga?

Wahshi kabisa!!
Vina siraha...
 
Dah! Yaan stend nzima inasambaratishwa na panya road kweli DSM hakuna wanaume
Kuna siku vilipanda daladala ya kigogo....vikamwamru dereva avipeleke chanika...akatii...abiria wote kimyaaaa na walishuka wote kituo kilichokuwa kinafuata
 
Baadhi ya askali waoga kuliko raia,bora serikali ipunguze mashart ya umiliki wa siraha kwa raia kuliko kutegemea askali waoga kiasi hicho.
 
Tukio hili limetokea leo saa 3:usiku Mbagala mwisho na shuhuda wa tukio hilo nikiwa mimi mwenyewe, Nikiwa njiani narudi nyumbani kulitokea taharuki kubwa baada ya tetesi kusikika kuwa Vijana watukutu maarufu kama PANYA ROAD wamevamia stand ya mbagala wakifanya wakipora mali na kupiga watu hovyo ndipo wananchi walianza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao.
KILICHONISHANGAZA
Nikiwa kwenye foleni nimeshuhudia Trafiki waliokuwa zamu wakitimka mbio huku wakivua kofia na mashati yao meupe na kubaki na nguo za ndani maarufu kama sing'lendi.
Swali nalojiuliza hawa askari wetu wanashindwa hata kufanya upepelezi wa mwanzo kujua adui yuko upande gani,ana siraha gani na atakabiliana naye vipi.
Chonde chonde wanaume wa Dar![emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hapo stendi hapakuwepo na wanaume?

Hivyo vitoto vitavamiaje stendi na kuanza kupiga na kupora watu?

Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Yaani watu mpo stendi mnaachia vitoto viwapore na kuwapiga?

Wahshi kabisa!!

[emoji115]Mkuu wewe ni mgeni huku JF???[emoji17].....kila siku tunavyolia na udhaifu wa wanaume wa Dar hapa JF huwa huoni??
 
Hawa jamaa wapo wangapi na wana silaha gani kiasi cha kukimbiza stendi nzima?
Isijekua watu wawili tu wanakimbiza wanaume 50, hata mawe watu mmeshindwa kuyakumbuka, hehehe! leo nimeamini kale kamsemo "wanaume wa dar"
 
Sielewi kabisa kwa kweli.

Yaani stendi nzima wanaume wazima wanakimbizwa na hivyo vitoto?

Hata vitofa wameshindwa kurusha?
 
Tukio hili limetokea leo saa 3:usiku Mbagala mwisho na shuhuda wa tukio hilo nikiwa mimi mwenyewe, Nikiwa njiani narudi nyumbani kulitokea taharuki kubwa baada ya tetesi kusikika kuwa Vijana watukutu maarufu kama PANYA ROAD wamevamia stand ya mbagala wakifanya wakipora mali na kupiga watu hovyo ndipo wananchi walianza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao.

KILICHONISHANGAZA
Nikiwa kwenye foleni nimeshuhudia Trafiki waliokuwa zamu wakitimka mbio huku wakivua kofia na mashati yao meupe na kubaki na nguo za ndani maarufu kama sing'lendi.
Swali nalojiuliza hawa askari wetu wanashindwa hata kufanya upepelezi wa mwanzo kujua adui yuko upande gani,ana siraha gani na atakabiliana naye vipi.
Daa!!
 
Hivi na mimi nikijifunza martial arts sijui hakuna ataenigusa eeh japokuwa msichana....[emoji124][emoji124]ngoja nikamatie fursa[emoji16]
 
Yaani ingekuwa chadema na Ukuta wangejaa kama nyuki kila kona na mazoezi juu tangu chadema wasitishe zoezi la ukuta kuna polisi umewaona wanafanya mazoezi kweli ? Panya road ni matukio ya muda kweli ina maana wameshindwa kabisa kuyakabili ? Haingii akilini kabisa .Ndio maana tunasema polisi wasiingie kwenye siasa mambo mengine yatakwama.
 
Back
Top Bottom