Panya Road waibuka tena Buza, wajeruhi watu na kuchoma mtoto Bisbisi ya kichwa

Panya Road waibuka tena Buza, wajeruhi watu na kuchoma mtoto Bisbisi ya kichwa

Ni lazima tujiulize maswali mengi, kwa nini kipindi cha JPM hakukuwa na hao panya road na kwa nini sasa?

Wameanza kwa mapanga na mwishowe mtasikia wanatumia bunduki, kwa sabb hao hawako peke yao, ni mkono mrefu huo,

Maana haiwezekani I we tuu ghafula baada ya utawala wa JPM kuisha, je, walikwenda wapi panya hao?

Polisi na panya road wanajuana, na huwenda ni maswahiba
umesahau bunduki za Kibiti wewe? Umesahau Panya Road walipambana na Makonda akiwa mkuu wa mkoa ?Umesahau yule kamanda aliyeleta msemo mtapigwa kama Mbwa koko alipambana na panya Road Temeke. ilikuwa zama gani?
Pambana na uhalifu acha siasa maji taka.
 
Hakuna kitu kibaya kama kushughulika na jambo linalolipuka lipuka linapunguza au kuondoa Amani kwa raia wema, "wakikamatwa wakathibishwa wasirudi uraiani wapelekwe magereza ya mbali wakalime huko kwa miaka 15,huku wakila wanacholima ili serekali isipate hasara"
 
Hili swala waende wakapate uzoefu kwa mzee wa kiraracha yy anajua walichofanya na mzee mkapa rip kuwamaliza majambazi hasa waliokuwa. Mby rpc akiwa kova au mwema kama sijakosea na rc alikuwa mramba majambazi wa chunya na kila eneo walikimbia hadi leo jombi hajulikani alipo miaka mid 90's hapo hakuna jambazi aalikuwa anakamatwa anapelekwa eti kituo cha polis
Ningekuwa mm ningefanya silent cleaning kama ya oparesheni tokomeza ya jk mpaka leo majangili wamepungua
Fanta moja ya kopo kwako mkuu.
 
Mzee wa kiraracha alikuwa waziri wa mambo ya Ndani enzi za mzee Ruksa na siyo Mkapa.
Enzi hizo Comando Yosso na Magenge mengine yalifyekelewa mbali
 
Nahisi kabisa kuna watu, wako nyuma ya kundi la hawa magaidi Lengo lao ni hii nchi isitawalike

mwenzenu naumia ninaposikia habari hizi.Sijajuwa hadi sasa nini hasa wanataka hawa mtoto jamani hawana imani hawa.
 
Polisi wanalewa wakiwa kazini!

Kwa staili hiyo msaada hakuna
 
Nahisi kabisa kuna watu, wako nyuma ya kundi la hawa magaidi Lengo lao ni hii nchi isitawalike

"walionyuma ya panya road ni upinzani". limesikika lifuasi limoja la sisiemu.
 
Ujangiri kuua tembo umerudi, upigaji kwenye miradi ya serikali, biashara ya madawa ya kulevya, panya road pia wamerudi, tutasikia mengi sana

Shisha nazo zimerudi kwa kasi tena wazi wazi haha
 
Kwenye taarifa ya habari walionesha wamekamatwa hao wametoka wapi tena[emoji848]
 
Back
Top Bottom