Panya road warudi Tena mchana huu

Hao polisi wangesikia kuwa ni CHADEMA wanafanya mkutano asee wangefurika na washawasha na risasi zakutosha.

Kikubwa inabidi wananchi wawe vigilant tu kama serikali imeamua kukaa kimya. Kamata hao panya choma mishaki achia mbwa wale.
Policcm ni maviiii kabisa [emoji90][emoji90][emoji90][emoji90][emoji90][emoji90][emoji90]
 
Huyo jamaa yako nadhani ni mhusika mie naongea na mdogo wangu wa kike, na mza mdogo wapo huko ndio wananiambia wamejifungia maana jamaa wamepita mtaani kwao we unakuja kubisha tu.
Mwambie awarekodi video
 
2019 Kuna mkubwa wao mmoja alipigwa mpaka kifo kule tabata darajani. So ilikuwepo tu sema walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo ya wanachakazwa tofauti na Sasa imekuwa Kama wanashirikiana na polisi
Hao ni mawakara na wateja wa ngada ( madawa ya kulevya) ya hukoo wa mzee wa msoga ,mama karudisha ngada mitaani sasa tunaona matunda yake .
 
Kwa maana Yako machinga ndio panya road siyo? Au magufuli ndiye aliyekuwa anawasaka wahalifu mtaani kwenu? Watendee haki machinga na usiwabebeshe zigo la panya road kwani walio wengi hawana muda na wizi Bali wanajishughulisha na biashara zao.
Na huyo magufuli alikuwa na watendaji aliowakasimu kazi ya kulinda raia na Mali zao! Je, wapo au wamestaafu au Wana mgomo? Au wanasubiri huyo magufuli wako awape amri ya kuwashughulikia panya road? Kama ndivyo basi ni sawa acha panya road watambe Hadi polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitakapopokea amri ya kufanyakazi kutoka Kwa magu!
 
Huyo aliyekupa taarifa ni mzushi na mwongo Sana! Jana majira ya kuanzia saa nane mchana watu walikatwa mapanga na kuumizwa mno kiasi kwamba walio wengi wamelazwa hospitali ya mwananyamala Kwa majeraha waliyoyapata. Binafsi niliwaona panya road wakiwa wamesambaratisha watu na kuvamia maduka na kupora bidhaa na pesa. Kuna mtaa unaitwa emii ndiko walikokimbilia kuelekea mashimoni. Sijasimuliwa nimeshihudia Kwa macho yangu! Vijana hao sio wa kuletea mizaha kwani ni hatari kuliko mbwa mwitu!
 
Hivi awamu ya Hayati Magufuli hii kitu ilikuwepo?
Kwani watu ni wale wale, askari wa kipindi kilee ndiyo Hawa walipo sasa.
Tunaomba askari watuonee huruma. Mtu anauwawa kwa sababu ya television kama yaliotokea Mwanza.
Wimbi la uhalifu limetamalaki kila mahali Tanzania.
Hivi kweli hivi mpaka Raisi alizungumzie
waziri mkuu yupo, waziri yupo, IGP yupo, RPC yupo, RCO yupo, OCD wapo,RC wapo, DC wapo, mtendaji kata wapo, watendi wa mtaa na vijiji wapo. Wabunge ndyo kabisaa hawajui ni nini wajibu wao
Hivi mnafanya mini.
Aibu yenu,
Naona mmezoa kazi,
Mnataka kufuatwafuata kama mwendazake alivyokuwa anafanya
Hii ndiyo TZ wakwepa majukumu.
 
Unasubiri uambiwe kujilinda?

wanaume wa Dar bana mna mambo flani ya kishosti shosti sana
Acha madharau mbwa wewe wanaume wa Dar ndio tunawafiraga nyie mbwa mnaotoka mikoani, Soma vizuri thread sio mimi mie nilikuwa town kwanza hata ukisoma hakuna nilipoonyesha balaa huko kwenye panya road wewe unajifanya hero kisa upo vichakani huko na unaandika kwenye simu yako vitu vya kujitamba kipuuzi.

Be humble watu wameumizwa unaleta kejeli zako za kitoto unadhani Hawa watu wote ni wajinga au hawana huo uwezo ? Jamaa mmoja aliwakabili lakini hakuwa na silaha akazuia panga amekatwa mkono Sasa unataka apambane vipi na amekuwa taken by surprise????

Those people wanakuvamia ukiwa barabarani unatoka kwenye shughuli zako, Sasa hapa mjini hakuna mashamba au sehemu za kukata mkaa kwamba utatembea na mapanga Kama huko mlipo msilete madharau yenu hapa mjini unatembea na peni tu Sasa ukivamiwa na watu wenye mapanga we hilo panga unalitoa wapi muda huo?

Kuweni na utu acheni kejeli za kijinga.
 
Maisha yamekuwa magumu.. juzi a day before Idd niliacha viatu nnje sijavikuta yani[emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa mara ya kwanza.. miaka yote niliyoishi hapa hili ndo tukio la kwanza



Sent from my SAMSUNG-SM-J327A using JamiiForums mobile app
 
Maisha yamekuwa magumu.. juzi a day before Idd niliacha viatu nnje sijavikuta yani[emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa mara ya kwanza.. miaka yote niliyoishi hapa hili ndo tukio la kwanza



Sent from my SAMSUNG-SM-J327A using JamiiForums mobile app
Imagine mtu anaona viatu, mie niliacha kopo la rangi la Lita nne na rangi ilikuwa imebaki kidogo sana Ila wakabeba hivyohivyo.

Unafika pahala unajiuliza ni ugumu wa maisha au mwizi ni mwizi tu?
 
Kuna kitu nyuma ya pazia sio bure.
Usikute huo ni mpango wa police kumfanya mama aonekane hafai? Waziri Masauni ni jana tu alikuwa Chanika akiwa na IGP Siro wakatoa matamko mengi iweje leo ijirudie. Kamanda Siro na Waziri wako mjitathmini. Tunaona kabisa mnamfanyia kusudi mama
 
serikali ya ccm inakwama wapi kwanini hao panya road wasitafutiwe paka road wanyooshwe
 
Nashukuru sana kwa mchango wako wa mawazo!

Kuna jambo moja natamani ujue, majukumu yote ya hao wateule wa rais uliowataja ni ya mh. Rais!!!!! Ni vile tu kwamba majukumu ni mengi na kwamba hawezi kuyatimiza peke yake ndiyo maana anachagua watu wa kumsaidia majukumu hayo!

Kama utendaji wao haumridhishi mh. Rais, anaowajibu wa kuwaondoa toka katika nafasi hizo na kuchagua wengine mbona nchi hii ni kubwa na watu wenye uwezo wengi tu???? Tunashindwa wapi?? Ilifika wakati RPC fulani akatamka wazi anatamani mh. Rais ampe u-IGP pengine aliona Kuna mambo hayaendi sawa! Kuchekeanachekeana kumekuwa kwingi mno! Kama vipi atengue achague wengine!

Mwendazake hakutufuatafuata kama unavyosema! Alitimiza wajibu wake! Hakucheka na wazembe! Ndiyo maana awamu yake ilifanikiwa! Sasa tunarudi nyuma! Nchi imekosa mwenyewe! Hakuna mwenye uchungu! Polisi wetu wanauwezo mkubwa sana kushinda panya road lakini kuna kuchekeana kwingi! Tunahitaji viongozi serious!
 
Paka road wapo wapi mpaka panya road wanazaliana kiasi hiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…