Panya Road wavamia nyumba za wakazi Kibaha, wapora na kujeruhi wananchi kadhaa

Panya Road wavamia nyumba za wakazi Kibaha, wapora na kujeruhi wananchi kadhaa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wananchi waliovamiwa na kundi la vijana Wahalifu wenye silaha mbalimbali maarufu Panya Road maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani wamesema vibaka hao waliwavamia kwa makundi huku wakisema hiyo ndio njia yao ya kupata rizki hivyo kila mtu atii amri ya kutoa anachoelekezwa.

Wakizungumza kwenye makazi yao baadhi ya wahanga na majeruhi wa tukio hilo wameeleza kuwa vijana hao walikuwa wakitamba kuwa hawana ajira na hiyo ndiyo ajira yao, na wao wanachotaka ni fedha, simu na mali nyingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema wahalifu hao wameiba vitu kadhaa na kujeruhi watu, na mmoja wa majeruhi ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Daktari wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi. Dkt Oscar Feruzi amesema wamepata wagonjwa 9 waliotokana an tukio hilo na wawili wamepelekwa Hospitali ya Muhimbili (Upanga) na Mloganzila.

Chanzo: Wasafi FM
 
1668769757282.png
 
Hakuna nchi isiyokuwa na jobless (watu wasiokuwa na kazi) Kwahiyo swala la kazi lisitumiwe kama kichaka cha kufanyia uhalifu.

Ukienda Zambia kuna wazambia kibao wasiokuwa na kazi, ukienda Botswana kuna wabotswana kibao wasiokuwa na kazi, ukienda Malawi, Zimbabwe, Kenya, Burundi, Rwanda mpaka huko America hali ni hiyo hiyo.

Mbona hakuna matukio ya kishenzi namna hii?

Inamaana ni wao tu peke yao ndo hawana kazi?

Mkuu wa mkoa wa Pwani na mkuu wa jeshi la polisi mkoani humo wafanye kama walivyofanya wenzao wa Dar es salaam nina imani hao mbwa koko watatubu na kurejea katika maisha ya kawaida ya kiraia.

Pia ulinzi shirikishi uanzishwe na uimarishwe.
 
Noma sana, nimesikia kuna msaada wa billion 209 zimetolewa na Germany kuwasaidia watanzania huku mtaani kuna vijana hawana ajira, hawana kazi, hata mitaji ya kufanyia biashara kwa vikundi pia hawana wanaishia kuwakaba watanzania wenzao tu na kuwaumiza na kuwarudisha nyuma, Serikali inafanya nini kuhusu hili itachukua maamuzi ya kuwaua au maamuzi gani ili kuwasaidia watoke kwenye huo ushetani? Kuwasaka na kuwafunga jela?
 
Haya polisi wahamie huko na kufanya kama walivyofanya kule temeke. Wazazi zaeni watoto mnaomudu kuwapa elimu bora ili waweze kufanikiwa maishani kwa kujituma.
sahihi kabisa shida ya watanzania wengi 90% wanazaa hovyo na kushindwa kuwalea watoto kwenye misingi mizuri ya kujitegemea.. WIZI ni matokeo ya mtu kuwa mvivu katika kufikiri na kutenda bila kuvunja sheria.
 
Wananchi waliovamiwa na kundi la vijana Wahalifu wenye silaha mbalimbali maarufu Panya Road maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani wamesema vibaka hao waliwavamia kwa makundi huku wakisema hiyo ndio njia yao ya kupata rizki hivyo kila mtu atii amri ya kutoa anachoelekezwa.

Wakizungumza kwenye makazi yao baadhi ya wahanga na majeruhi wa tukio hilo wameeleza kuwa vijana hao walikuwa wakitamba kuwa hawana ajira na hiyo ndiyo ajira yao, na wao wanachotaka ni fedha, simu na mali nyingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema wahalifu hao wameiba vitu kadhaa na kujeruhi watu, na mmoja wa majeruhi ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Daktari wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi. Dkt Oscar Feruzi amesema wamepata wagonjwa 9 waliotokana an tukio hilo na wawili wamepelekwa Hospitali ya Muhimbili (Upanga) na Mloganzila.

Chanzo: Wasafi FM
Vijana wote wavivu wa kufanya kazi halali kama hawa panya road Jeshi la polisi wauweni wote, nchi inaonekana ina watu wengi kumbe 80% hawana faida kwenye nchi ...kila wakati ni kutengeneza matukio tu yasiyo na faida ...uaaa wote shenzi.
 
Back
Top Bottom