Panya Road wavamia nyumba za wakazi Kibaha, wapora na kujeruhi wananchi kadhaa

Panya Road wavamia nyumba za wakazi Kibaha, wapora na kujeruhi wananchi kadhaa

Hawa panya road ni kukamata na kupeleka Russia [emoji635]
Wawekwe frontline, that’s all walahi [emoji3062]
Uraaaa [emoji635][emoji635][emoji635]
 
Washenzi tu ndio wanaamini kama wapwani ndio panya road au wasio na elimu ndio panya road pekee,ila ukweli wanaujua lakini ni kutukana watu tu kwa kuwa ndio wanavyofundishwa kuanzia nyumbani hadi huko kwenye hizo elimu zao za ushindani
 
Hakuna nchi isiyokuwa na jobless (watu wasiokuwa na kazi) Kwahiyo swala la kazi lisitumiwe kama kichaka cha kufanyia uhalifu.
Ukienda Zambia kuna wazambia kibao wasiokuwa na kazi, ukienda Botswana kuna wabotswana kibao wasiokuwa na kazi, ukienda Malawi, Zimbabwe, Kenya, Burundi, Rwanda mpaka huko America hali ni hiyo hiyo.

Mbona hakuna matukio ya kishenzi namna hii?
Inamaana ni wao tu peke yao ndo hawana kazi?

Mkuu wa mkoa wa Pwani na mkuu wa jeshi la polisi mkoani humo wafanye kama walivyofanya wenzao wa Dar es salaam nina imani hao mbwa koko watatubu na kurejea katika maisha ya kawaida ya kiraia.

Pia ulinzi shirikishi uanzishwe na uimarishwe.
Dar walifanywa nini mkuu?
 
Kibaha, Kongowe eneo lote la VETA mpaka Kigelo.
Eneo lote la halmashauri ya kibaha mji sio salama. Kibaha vituo vya polisi vinafungwa saa 12 jioni. Hakuna patrol Wala nini.
Wananchi wangeweza kuchoma panya road wanne tu nadhani wangehamia chalinze.
 
Samahani jamani Mimi naomba niulize, hivi kazi ya Polisi, wanajeshi na wanaopigana ngumi ulingoni bila ugomvi si ndo hii..tuache mambo ya sijui wanajeshi ni watu wa kulinda nchi sijui nini..kimsingi waungane wamwagwe mtaani wakawasake Hawa watu..sasa Kuna haja Gani ya wao kulipwa fedha za Kodi ya wavuja jasho na matukio ya kihalifu yanaongezeka Kila siku
 
Wananchi waliovamiwa na kundi la vijana Wahalifu wenye silaha mbalimbali maarufu Panya Road maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani wamesema vibaka hao waliwavamia kwa makundi huku wakisema hiyo ndio njia yao ya kupata rizki hivyo kila mtu atii amri ya kutoa anachoelekezwa.

Wakizungumza kwenye makazi yao baadhi ya wahanga na majeruhi wa tukio hilo wameeleza kuwa vijana hao walikuwa wakitamba kuwa hawana ajira na hiyo ndiyo ajira yao, na wao wanachotaka ni fedha, simu na mali nyingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema wahalifu hao wameiba vitu kadhaa na kujeruhi watu, na mmoja wa majeruhi ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Daktari wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi. Dkt Oscar Feruzi amesema wamepata wagonjwa 9 waliotokana an tukio hilo na wawili wamepelekwa Hospitali ya Muhimbili (Upanga) na Mloganzila.

Chanzo: Wasafi FM
Wameula wa chuya
 
Back
Top Bottom