Panya wa Kichina wamevamia Dar es Salaam. Hawali sumu yao pia wanajua mtego. Serikali itusaidie

Panya wa Kichina wamevamia Dar es Salaam. Hawali sumu yao pia wanajua mtego. Serikali itusaidie

Hao panya sio wale ambao wapo gongo la mboto kwa sana haswa maeneo ya karibia na Kampala university. Huwa na midomo mirefu na wanatoa visauti flani vya kukera na sometimes wanang'ata..

Kama ni hao ni wa muda sana na baadhi ya watu wa gomz huamini ni panya wa maabara
 
Kuna panya wamevamia Jiji la Dar Es Salaam.

Hawa panya hata uwatege kwa sumu ya panya hawali. Wanajua mitego yote ya panya. Na ukimfuata bila tahadhari anakurukia kukung'ata.

Huwezi kuwanasa labda uwapige na nyundo au fimbo.

Inadaiwa ni panya wa Kichina na Wametoka China. Wanapiga kelele sana na Wanaitana.

Serikali isaidie kuwatokomeza kama walivyo punguza Kunguru.

Nilibahatika kuwaona. Wana mdomo mrefu...
View attachment 3279342
Panya wakichawi tu hao...

Tumia ule mtego wa kitabu utawanasa kilaini tu
 
Tatizo lenu hakuna mnachojifunza kwa wengine, yaani mataifa mengine
Kuna mifano mingi sana
Ila kwa mfano Australia
Wao wanachunga sana ardhi yao na kuwalinda wakulima pia.

Kila kinachoingia kwao wanakagua sana, iwe bandari, Anga na hata majini.

Utakaguliwa sana hata kama una matunda yanatupwa

Sasa makontena ya Mchina lazima yanakuwa na panya na hata nyoka ila nyie mnaangalia mzigo una bidhaa gani tosha

Wajapani walipeleka Samaki flani eti ni mambo ya Imani USA
Wakawa wakubwa na kuzaana manyumbani kwao wakaanza kuwatupa Mtoni.
Matokeo yake wakawala samaki wengine wote na kusababisha hasara kubwa
Hawa watu wanaingiza kila kitu maana wanakula kila kitu kasoro Mawe tu
Msipowadhibiti na kuwakagua wataingiza kila aina ya viumbe na mwisho wake baada ya miaka kadhaa mashamba yatavamiwa na kuharibu mifugo

Serikali Sikivu haya kazi kwenu
 
Nimewamaliza kupitia hiki kitabu chenye gundi kama kuna mpenyo wanapita wategee lazima anase tu sababu ana kawaida ya kuingia na kutoka nje ya nyumba
 

Attachments

  • 17426275071433544716388787491605.jpg
    17426275071433544716388787491605.jpg
    272.9 KB · Views: 18
Tumia mtego wa kufyatua anaponasa mmoja, uoshe mtego harufu itoke, tega Kwa mara nyingine
Ooh kumbe?

Ndio maana tangu nimnase yule mwenzao mmoja, mpaka leo sijamnasa mwingine na kila siku na wabadilishia chakula pale, nilishanunua mpaka mishkaki awaingii tena mtegoni.. kumbe mpaka nioshe huo mtego harufu ya mwenzao itoke?
 
Si mlisema China ndo rafiki bora duniani kuliko mabeberu na kila kitu kuanzia miradi apewe yeye?

Imekuaje tena? 🤔
 
Kuna panya wamevamia Jiji la Dar Es Salaam.

Hawa panya hata uwatege kwa sumu ya panya hawali. Wanajua mitego yote ya panya. Na ukimfuata bila tahadhari anakurukia kukung'ata.

Huwezi kuwanasa labda uwapige na nyundo au fimbo.

Inadaiwa ni panya wa Kichina na Wametoka China. Wanapiga kelele sana na Wanaitana.

Serikali isaidie kuwatokomeza kama walivyo punguza Kunguru.

Nilibahatika kuwaona. Wana mdomo mrefu...
View attachment 3279342
Vita vya Uchumi
 
Paka akikutana na hawa panya anaingia uvunguni kujificha.
Hawa panya huku mtaani wanaitwa "panya wa mama sa100"
 
Kuna panya wamevamia Jiji la Dar Es Salaam.

Hawa panya hata uwatege kwa sumu ya panya hawali. Wanajua mitego yote ya panya. Na ukimfuata bila tahadhari anakurukia kukung'ata.

Huwezi kuwanasa labda uwapige na nyundo au fimbo.

Inadaiwa ni panya wa Kichina na Wametoka China. Wanapiga kelele sana na Wanaitana.

Serikali isaidie kuwatokomeza kama walivyo punguza Kunguru.

Nilibahatika kuwaona. Wana mdomo mrefu...
View attachment 3279342
Haya nimajini sio panya hata serikali itashindwa kuwadhibiti mwagia maji ya upako
 
Back
Top Bottom