JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Papa Francis (85) hakuitaja moja kwa moja Urusi lakini aliposema kuwa mashambulizi ya Mji wa Mariupol yamekuwa ya kinyama na kusababisha watu kuhamishwa kutoka katika mji huo ni wazi anakosoa mashambulizi yanayoendelea.
“Ninasikiika na kulia kwa watu wan Ukraine hasa wale ambao ni dhaifu, wazee, watoto… ni habari ya kusikitisha kuona watu wakihamishwa katika mji wao,” anasema Papa.
Kulingana na vyombo vya habari vya Urusi, jumla ya raia 46 wamehamishwa kutoka eneo lililo karibu na kiwanda cha chuma kilichozingirwa cha Azovstal katika mji wa bandari wa Mariupol.
Source: English Alarabiya