Papa Francis akutwa na Nimonia

Papa Francis akutwa na Nimonia

Ndugu zangu Watanzania,

Vatican imethibitisha kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameugua nimonia (bilateral pneumonia) hali inayohusisha maambukizi kwenye mapafu yote mawili.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Vatican Madaktari wake wamebaini ugonjwa huo baada ya vipimo vya kitabibu na kwa sasa anapatiwa matibabu maalum huku hali yake ikiwa chini ya uangalizi wa karibu.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 87 amekuwa na changamoto za kiafya kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na matatizo ya kupumua na maumivu ya mifupa hata hivyo Vatican imesisitiza kuwa anaendelea kupokea huduma bora za kitabibu na anaendelea vizuri matibabu.

Maelfu ya Waumini wa Kanisa Katoliki duniani kote wameendelea kumuombea afya njema huku Viongozi wa dini na Viongozi wa mataifa wakionesha mshikamano na kumtakia ahueni ya haraka.
#MillardAyoUPDATES

View attachment 3241793
Pole sana Papa...unatakiwa ustaafu sasa
 
Anatupima ili imani zetu zionekane kwa Matendo
Ili kubainisha waumini wa kweli na wanafiki
Mungu mjuzi wa vyote tangu mwanzo na hata milele, Anakupima nini asichokijua?

Kwani huyo Mungu hawezi kujua waumini wa kweli na wanafiki, Hadi awapime?

Au huyo Mungu hajui mambo yote?
 
Back
Top Bottom