Papa Francis akutwa na Nimonia

Papa Francis akutwa na Nimonia

Afya ya Rais wa Vatican na Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani. Papa Francis ipo Mashakani. tumkumbuke kwenye sala zetu
 
Mimi ni Catholic ila nawazaga sana kwanini walikataa yule mcameroon kuwa papa hali ya kuwa walisema moshi umetokea kwake, asubuhi wakasema moshi ulikuwa mweusi mara sijui vinini aaghh wana ubaguzi mchakato wa kumpata papa kama tu uchaguzi wa Tz
 
Atakua ameshafariki na sasa wanatafuta namna ya kutangaza kifo chake!!

Alianza kusema sabato ni jumamosi badala ya jp!!

Rip in advance pope!!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Vatican imethibitisha kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameugua nimonia (bilateral pneumonia) hali inayohusisha maambukizi kwenye mapafu yote mawili.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Vatican Madaktari wake wamebaini ugonjwa huo baada ya vipimo vya kitabibu na kwa sasa anapatiwa matibabu maalum huku hali yake ikiwa chini ya uangalizi wa karibu.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 87 amekuwa na changamoto za kiafya kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na matatizo ya kupumua na maumivu ya mifupa hata hivyo Vatican imesisitiza kuwa anaendelea kupokea huduma bora za kitabibu na anaendelea vizuri matibabu.

Maelfu ya Waumini wa Kanisa Katoliki duniani kote wameendelea kumuombea afya njema huku Viongozi wa dini na Viongozi wa mataifa wakionesha mshikamano na kumtakia ahueni ya haraka.
#MillardAyoUPDATES

View attachment 3241793
Sasa hivi anaendeleaje?

View: https://x.com/ImtiazMadmood/status/1895171174016876682
 
Kiswahili kigumu, Kumbe Pneumonia kiswahili chake ndio NIMONIA?
 
Mimi ni Catholic ila nawazaga sana kwanini walikataa yule mcameroon kuwa papa hali ya kuwa walisema moshi umetokea kwake,
Nani alikataa? Huo moshi unamtokea anayechaguliwa au unatutokea watu tuliopo nje kusubiri aliyechaguliwa? Vitu vingine kama mtu hujui heri kupiga kimya
 
Back
Top Bottom