Papa Francis asihi waliotekwa waachiwe huko Israel na Palestina

Papa Francis asihi waliotekwa waachiwe huko Israel na Palestina

HISTORIA KWA UFUPI , mwaka 1948 wapalestina walipewa eneo kubwa tu kuliko waisrael ila tamaa ikawaponza wakalitaka eneo dogo la waisrael wakidai wanataka kuwaondoa wayaudi kwenye uso wa dunia , bas mamb yakawa kinyume wapalestina wakapigwa na kuporwa wao eneo , miaka michache baadae wapalestina na waarab wakaanzisha mapambano mapya kwa kuivamia israel ila wakapigwa na kuporwa tena eneo jingine , pia wapalestina wamekuwa wakijichanganya mpk leo wanaanzishaga ugomv hlf wanaishia kuporwa maeneo ba hawajifunzi , kipind waisrael wanapambana kujenga taifa , wapalestina walipambana kuiondoa vizaz vya wayaudi hapo mashariki ya kati huku wakisahau kusau kuwa wao si taifa linalotambuliwa kimataifa
Kumbeeee! Mimi siku zote nadhani Israel ndio mchokozi kujitanua. Kumbe muarabu ndio kima. Basi wacha wachezee kipigo kitakatifu.
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, katika matamshi yake makali tangu kuanza kwa mzozo kati ya Palestina na Israel, ametoa wito wa kuachiliwa kwa Mateka wote waliochukuliwa na wanamgambo wa Hamas na kusema Israel ina haki ya kujilinda.


Mtandao wa DW Swahili umeripoti kuwa akiongea mwishoni mwa hadhara yake ya kila wiki kwa maelfu ya Watu katika uwanja wa St. Peter, Papa Francis ameelezea pia wasiwasi wake juu ya kuzingirwa kwa Israel na Gaza.

"Ninaendelea kufuatilia, kwa uchungu na wasiwasi kile kinachotokea Israel na Palestina, Watu wengi sana wameuawa na wengine kujeruhiwa, naziombea Familia zilizoshuhudia siku ya sikukuu ikigeuka kuwa siku ya maombolezo na ninaomba kwamba Mateka waachiliwe mara moja.”

"Ni haki ya wale wanaoshambuliwa kujilinda, lakini nina wasiwasi mkubwa na mzingiro mzima wa Wapalestina wanaoishi Gaza, ambako pia kumekuwa na wahasiriwa wengi wasio na hatia.”

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya ndege usiku kucha katika viunga vya ukanda wa Gaza, huku vita vyake dhidi ya kundi la Hamas vikiingia siku ya tano leo Jumatano na zaidi ya Watu 2,200 wameuawa katika vita hivyo kwa pande zote huku vifo vikihisiwa kuongezeka.
Huyo papa tangu aruhusu ndoa za mashoga nilishamtoaga thamani.
 
Nimesoma uzi na comments zake zote. Nilichokiona hapa watu wengi wanacomment kwa chuki tu dhidi ya papa, lakini alichokiongea ni hekima ambayo tangu mgogoro huu umeanza wengi wameikosa. Wengi wanaozungumza, wakubwa kwa wadogo, wameishia kuegemea upande mmoja pekee lakini papa kawa neutral kabisa.

Neutrality ya papa ipo wazi kiasi cha kila aliyesoma uzi kuelewa. Ndo maana katika attackers wote kwenye uzi huu hakuna aliyeweza kunukuu kauli ya papa anayoipinga kwa sababu ukipinga kwa kunukuu hoja lazima utapuyanga tu.

Wakati wenye kuegemea upande mmoja wakizungumza tunapiga kelele wawe neutral kwenye mzozo, halafu walio neutral nao tunawatusi wao binafsi kwa chuki zetu za kichawi bila hata kuzingatia walichokizungumza. Waafrika (hasa wabongo) sijui tulirogwa na nani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom