Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 450
- 3,368
Kauli hii inakuja muda mchache baada ya Donald Trump kudai Papa Leo XIV ni dhaifu, hapendezwi na uongozi wake kwakuwa si mfuasi wa MAGA, na kwamba amekuwa anapingana na sera zake.
Undani wa kauli ya Trump unaweza kuupata hapa >>> Trump: Papa Leo XIV ni dhaifu, simshabikii
"Nadhani watu wanaosoma wataweza kufikia hitimisho lao wenyewe: mimi si mwanasiasa, sina nia ya kuingia kwenye mdahalo naye. Badala yake, hebu daima tutafute amani na kukomesha vita. Siogopi utawala wa Trump.
Nazungumzia Injili, mimi si mwanasiasa. Sidhani kama ujumbe wa Injili unapaswa kutumiwa vibaya jinsi baadhi ya watu wanavyofanya.
Nitaendelea kupaza sauti dhidi ya vita, kujaribu kukuza amani, na mazungumzo ya pande nyingi kati ya mataifa ili kutafuta suluhisho sahihi la matatizo. Ujumbe wa Kanisa ni ujumbe wa Injili, heri wapatanishi; sioni jukumu langu kama mwanasiasa, sitaki kuingia kwenye mdahalo naye. Watu wengi sana wanateseka duniani."