Papa Leo XIV amemteua Mhashamu Wilbroad Kibozi kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki Kondoa

Papa Leo XIV amemteua Mhashamu Wilbroad Kibozi kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki Kondoa

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Mhashamu Wilbroad Kibozi kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki Kondoa, kufuatia kifo cha aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo, Mhashamu Bernardin Mfumbusa.

Kabla ya uteuzi huo, Askofu Kibozi alikuwa akihudumu kama Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Jumatano Aprili 22, 2026 na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania, Angelo Accattino wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya mazishi ya marehemu Askofu Mfumbusa, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Jimbo Katoliki Kondoa.

Mhashamu Mfumbusa alifariki dunia Aprili 14, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Screenshot 2026-04-22 200529.png
 
Back
Top Bottom