Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
- Thread starter
- #141
Ni sahihi kabisa.Hayo maandishi yalikuwepo na hakuna aliyeyafahamu isipokuwa waislamu mwanzo kabisa pale Baghdad na baadae wakavitafsiri kwa lugha ya kiarabu na kutunza kila walichokiona cha asili.Vipi na kuhusu Tourat, Injil na Zaburi nazo zilikuwa katika lugha ya Kiislamu (Kiaarabu) kwanza ndo baadaye vikatafsiriwa kwenda Kiebrania, Kigiriki na Kilatini??? kwamba enzi za Musa na zama za Yesu uislamu ulishakuwa na vyuo vyake???
Hulagu ambaye ni mkristo aliyetokea jamii ya kihindi na alikuja kuchoma moto hazina kubwa ya maandishi ya kale na waislamu wachache ndio walioviokoa vilivyobaki na kuviokota vilivyotupwa mtoni na ndivyo ambavyo vingi vimetufikia sisi baada ya kutafsiriwa.
Kwa ufupi katika historia ya elimu duniani hakuna kichochoro cha kukwepa wema wa uislamu katika kuiritihisha dunia kilicho bora.