Papa wa Kanisa Katoliki anakuwa Mtakatifu kwa misingi ipi?

Papa wa Kanisa Katoliki anakuwa Mtakatifu kwa misingi ipi?

Kuna Kanisa 'Takatifu' Moja tu Katoliki la Mitume Duniani ambalo humo Kuna Watakatifu sio mmoja ni Wengi Wanapatikana.
Sasa huko mliko kama mna Uhakika hakuna Watakatifu basi ni wakati Sasa Wa Kukata shauri Rudini
Katika KANISA MOJA TAKATIFU LA MITUME!!
Amina.Barikiwa sana Mtumishi.
 
Nawaza utakatifu anapewaje kiongozi kibinadamu tu?

Je, kuna ushahidi wa maandiko unaoonesha kuwa Papa anakuwa mtakatifu automatically?

Na Kama Roho mtakatifu anaongea na watu wake kipi wafundishe why wampangie cha kufundisha dunia nzima?
Bwana mkubwa, naomba nikujibu hivi, Kanisa Katoliki linapomwita kiongozi wake "Baba Mtakatifu", haina maana kuwa yeye ni Mtakatifu.Isipokuwa kiti anachokalia ni kitakatifu, hivyo Kuitwa "Baba Mtakatifu" Kunamwajibisha yeye kujibidiisha kuutafuta Utakatifu.Kwa kuzingatia kuwa yeye ni binadamu na anaweza kukosea Papa naye huwa anaungama ili kufanya Upatanisho kati yake na MUNGU,Mara kadhaa tumekuwa tukimsikia Papa Francis akisema "Yeye si mkamilifu,ni mtu mwenye dhambi",Kwa taarifa yako Papa Francis anaungama mara mbili kwa wiki.Tafsiri yake ni Nini hapo?,Ni kwamba anajua kuwa kile kiti kinamdai yeye kuwa Mtakatifu,sasa anajitahidi kutubu mara kwa mara ili kudumisha hali Njema ya Kiroho.Ndio maana basi sio Mapapa wote waliotangazwa kuwa Watakatifu sababu inaweza kuwa ni kutokana na kutotimiza matakwa ya MUNGU ktk Utumishi wao.Nikwambie tu ndugu yangu kuwa Kila siku huwa tunaalikwa kumuombea Baba Mtakatifu ili aweze kushinda nguvu za yule mwovu.Kwa kuhitimisha ni kwamba Baba Mtakatifu haimaanishi kuwa yeye ni Mtakatifu Bali kiti au cheo kile ni kitakatifu hivyo kinamdai yeye kuishi Kitakatifu.

Nikutakie Heri ya Mwaka mpya wa 2022.
 
WAKATOLIKI wana mwanadamu waliempa jina lenye wadhifa na wasifu wa Mungu peke yake, yaani " Baba Mtakatifu"

Soma: Yohana 17:11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

Umeona hiyo aya inavobainisha kuwa "Baba Mtakatifu" ni jina la Mungu? Lakini Wakatoliki wana baba yao mtakatifu mwingine!!!!!? KUFURU!.

ya hii ya 9, Mungu kakataa kuwa na ubia ktk jina lake la mamlaka linalobeba wadhifa wake. Kumwita mtu baba Mtakatifu na kiongozi mkuu wa dini ni KUFURU.
Mwenye masikio na asikie ambayo roho awaambia Wakatoliki

Mathayo 23:9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.

Zab 16:3​

Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Ninavyojua mimi watakuja na matusi, kejeli na kujikweza na si maandiko. Wakileta maandiko ni tag
 
Wakatoliki Ni warumi Tu Yani wale kina gladiators,Spartans,Greek gods, Olympus
 
Una swali zuri mkuu na huu ni mjadala mpana lakini kwa hali ilivyo usitegemee kupata majibu humu labda ungewauliza mapadri wale jamaa wanasoma sana huenda ukaokota chochote kitu lakini kwa hii jf sidhani maana wengi watajibu kwa hisia tu

Zab 16:3​

Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
 
Kuna Kanisa 'Takatifu' Moja tu Katoliki la Mitume Duniani ambalo humo Kuna Watakatifu sio mmoja ni Wengi Wanapatikana.
Sasa huko mliko kama mna Uhakika hakuna Watakatifu basi ni wakati Sasa Wa Kukata shauri Rudini
Katika KANISA MOJA TAKATIFU LA MITUME!!
Rumi haijawahi kua Takatifu .

Mpaka Yesu anazaliwa, Rumi ilikua ikitawala kiserikali ( haikua na Dini).

Rumi hiyo ya kiserikali ilikua ina Sheria zake, tamaduni zake , mila zake , kama vile Kuabudu mungu Jua, Sanamu za wakuu wake, Miti ( huu unaotumika kwenye Christmas) kwakua ni mti uliokua unahimili hali ya ukame, ivo ukachaguliwa kama mungu wamimea, waliabudu mungu mwanamke n.k.

Yesu anazaliwa mpaka anaanza kazi zake, watu wakamfuata ,nao wakaitwa WAKIRSTO ..yaan watu wa Yesu Kristo. .

Yesu anasulubiwa, anaacha wanafunzi wanaichapa injili Dunia .

Aliyekua Papa wa Rumi ya kiserikali COSTANTINE , Baada yakuona mapambano dhidi ya ukrsito yameshindwa na kwamba Tamaduni za Roma zinaelekea kupotea.

aliamua mwenyewe ,kujiingiza katika Ukristo na kua KIONGOZI MKUU wakwanza wa Rumi kua Mkristo.

Ni katika huo Ukristo wake aloingia, ndio akafanikiwa baadae kwanza, kuitenga Jumapili kua ibada Dunia nzima( akijua kwa kuiabudu siku hiyo ya jumapili ya mungu Jua ), Kua Krismas ifanyike 25 /12 kuendelea kusherekea mungu wa mimea n.k n.k .

Sasa nn kilichotokea ???

Baada ya Rumi sasa kua na mamlaka mbili za kiserikali na Kidini , wapo wakrsto baadae waloona hapana, Rumi inaenda kinyume na Mafundisho ya Yesu .

Wakristo hao wakajitoa kwa Rumi nakuanzisha makanisa yao ,namiaka ilivyozidi kusogea wakazidi kujiondoa na kuanzisha makanisa ndo ambayo Leo yapo.

ROMA, HAIJAWAH KUA KANISA LA MITUME.

LABDA KAMA HUIJUI HISTORIA,

wazijua zama za Giza????

Ambapo Rumi hii , ilikua Wakristo zaidi ya million???..( gugo ).

Rumi iliua Wakristo mpaka mwaka 1798 ambapo Papa alichukuliwa mateka na Majeshi ya ufaransa , ndo ukawa mwisho wa mauaji ya Wakristo.

Mambo ni mengi , Ingia tafuta vitabu usome !!..... ROMA HAIJAWAH KUA KANISA LA MITUME.
 
Papa Francis sio mtakatifu na wala sio kila papa ni mtakatifu ndio maana kuna mapapa wachache ambao tunawaita watakatifu. Sababu ni kwamba Cheo cha Upapa ndio Cheo kitakatifu kwa kuRefer maneno ya Yesu mwenyewe alipomteua Peter kua papa wa kwanza Mathayo 16:18
[18]Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa (Roman Catholic)langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Waafrika bana. Roman
 
HISTORIA YA KUGAWANYIKA KWA KANISA KATHOLIKO MWAKA 1054.

Hapa kuna kielelezo muhimu sana kuhusu yale tunayoandika kuhusu Historia ya Kanisa. Jana, tuliandika makala kuhusu Mtakatifu Catherine wa Alexandria. Mara kadhaa tumeeleza kuwa katika 250 ya mwanzo wa Kanisa, kulikuwa na Makanisa au Majimbo Makuu manne tu dunia nzima.

Makanisa au Majimbo hayo yalikuwa ni: Kanisa la Yerusalemu, Kanisa la Antiokia, Kanisa la Rumi na Kanisa la Alexandria. Kila Kanisa lilikuwa na Askofu Mkuu (Papa) ambaye alikuwa na mamlaka juu ya Makanisa kadhaa na Maaskofu kadhaa chini yake katika jiografia ya eneo lake.

Maaskofu Wakuu (Mapapa) wa Makanisa hayo walikuwa na hadhi sawa, ingawa kwa kadiri miaka ilivyozidi, Askofu Mkuu wa Rumi (Papa) akawa anapewa nafasi ya kwanza (first among the equals) miongoni mwa Maaskofu Wakuu wanne waliokuwa sawa. Sababu zilikuwa mbili: Kanisa la Rumi liliwahi kuchungwa na Mtume Petro, ingawa siyo yeye ambaye ndiye aliyekuwa amelianzisha; na pili, Rumi yalikuwa ndio Makao Makuu ya Dola ya Kirumi.

Kati ya mwaka 225 hadi 281, Kanisa la Constantinople (sasa Istanbul, Uturuki) likaanza kupata hadhi. Baada ya Mfalme Constantine kuhamisha Makao Makuu ya Dola ya Kirumi kutoka Rumi kwenda Mji wa Constantine (Constantinople), Uturuki, Kanisa la Constantinople likapewa hadhi na kuwa kama Makanisa hayo mengine na hivyo Makanisa au Majimbo Makuu kuwa matano na kuwa na Maaskofu Wakuu watano wenye hadhi sawa.

Kanisa la Yerusalemu, Kanisa la Antiokia, Kanisa la Alexandria na Kanisa la Constantinople yalikuwa Upande wa Mashariki ambapo Lugha yao Kuu ilikuwa ni Kiyunani (Kigiriki) na pia kiutawala katika siasa za dunia yalikuwa sehemu ya Dola ya Kirumi ya Mashariki (Byzntine). Kanisa la Rumi lilikuwa Magharibi na Lugha iliyokuwa inatumika ilikuwa ni Kilatini. Kisiasa lilikuwa sehemu ya Dola ya Kirumi ya Magharibi.

Hadi kufikia mwaka 1054, Kanisa lilikuwa likijulikana kama Kanisa Katholiko. Katholiko linatokana na neno la Kigiriki likiwa na maana ya yote, iliyo kila mahali, iliyo popote, ya dunia nzima, nk. Neno Catholico lilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na Askofu Mkuu Ignatius wa Antiokia akilielezea Kanisa katika Waraka wake kwa Kanisa la Symirna miaka ya mwanzo kabisa ya Ukisto. Hadi kufika mwaka 300 BK (Baada ya Kristo), Kanisa lote likajulikana kama Kanisa Katholiko!

Tofauti za kitheologia, kifalsafa, kisiasa, kijiografia na kiutamaduni zilichangia kuanza kwa Mgogoro wa Kanisa yapata mwaka 700 BK (Baada ya Kristo). Mgogoro ule ulidumu kwa muda wa zaidi ya miaka 300 bila kupatiwa ufunguzi wa kudumu. Ubabe wa viongozi wa baadaye ulipelekea Kanisa kugawanyika kabisa mwaka 1054 baada ya Papa wa Kanisa la Rumi kumtenga Papa wa Kanisa la Constantinople na Papa wa Kanisa la Constantinople naye kumtenga Papa wa Kanisa la Rumi. Baada ya Mapapa wa Kanisa la Rumi na Constantinople kutengana, Kanisa Katholiko likawa limegawanyika matika sehemu mbili.

Makanisa madogo ya Magharibi yaliliuunga mkono Jimbo Kuu au Kanisa la Rumi na Askofu Mkuu wa Rumi (Papa). Makanisa hayo yakajiita Western Roman Catholic Church (Kanisa la Katholico la Kirumi la Magharibi) ambalo kwa kifupi likajulikana kama Roman Catholic Church (RC).

Majimbo Makuu matatu ya Yerusalemu, Antiokia na Alexandria pamoja na Makanisa madogo chini yao yaliuunga mkono Jimbo Kuu au Kanisa la Constantinople na Askofu Mkuu (Papa) wa Constantinople. Makanisa hayo yakajiita Eastern Orthodox Catholic Church (Kanisa Katholico la Kiothodoksi la Mashariki). Kwa kifupi yakajulikana kama Eastern Orthodox au Orthodox Church. Waliongeza neno Orthodox ambalo ni la Kigiriki likiwa na maana ya iliyo ya kweli. Hii ilikuwa ni namna ya wao kuelezea uasi wa kitheologia wa Kanisa la Magharibi kwani walikuwa wanalituhumu kuasi maamuzi ya Mitaguso (Mikutano Mikuu) au Synod za Kanisa zima kwa kuchakachua Imani ya Nikea.

Kanisa la Roman Catholic lileendelea kukumbwa na migawanyiko kuanzia mwaka huo wa 1054 kama ifuavyo: Lilizaliwa Kanisa la Waldensia ingawa halikuwa kubwa sana na hadi sasa lina waumini wasiozidi 50,000 nchini Ufaransa. Mwaka 1400s lilizaliwa Kanisa la Umoja wa Ndugu (Moravian Church); kuanzia mwaka 1525 zilianza hatua za kuandaa Katesimo na hatimaye kuzaliwa Kanisa la Kilutheri. Sambamba na Kanisa la Kirutheri lilizaliwa Kanisa la Mennonite na Presbyteria. Baadaye lilizaliwa Kanisa la Uingereza (Kanisa Anglikana). Kanisa la Methodist lilimeguka kutoka Kanisa Anglikana. Madhehebu ya Kibatisti ni sehemu ya mgawanyiko uliozaa Mennonite na Presbyteria.

Kanisa Catholiko la Kiothodoksi halijawahi kugawanyika tangu wakati ule. Kanisa la Ethiopia ni sehemu ya Kanisa la Orthodox pamoja na Kanisa la Misri (Coptic). Makanisa mengine ya Orthodox ni Russian Orthodox, Greek Orthodox, Cyprus, Ukraine, Rumania, Syriac, nk. Hadi kufikia mwaka 1961, kulikuwa na waumini wa Orthodox Catholic Church dunia nzima wapatao zaidi ya Milioni 122.

Matawi yote ya Kanisa Katholiko yaliyizaliwa wakati wa mgawanyiko wa Kanisa wa mwaka 1054 na yaliyizaliwa baada ya Kanisa la Roman Catholic Church kugawanyika ni sehemu ya Kanisa Katholiko hata kama mengine hayajiiti hivyo mara kwa mara kwa mara. Makanisa hayo ni yale yote yanayokiri Imani ya Mitume, Imani ya Nikea na Ukiri wa Athanasio. Makanisa hayo ni pamoja na Roman Catholic Church, Eastern Orthodox Catholic Church, Waldensian Church, Moravian Church, Lutheran Church, Anglican Church, Mennonite Church na Presbyterian Church.

Je, ni jambo gani kimekushangaza na kukufurahisha? Je, ni jambo gani limekuhuzunisha?

NB: Angalia taarifa ya Muhidin Issa Michuzi hapo chini kuelezea ujio wa Papa wa Kiothodoksi nchini.

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula ambaye ndiye maandishi wa makala hizi, ni Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani. Pia, ni Mhadhiri wa Theologia, Falsafa, Soshologia, Literature, Missiologia, Historia ya Kanisa na Utafiti. Amefundisha masomo hayo kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu, St. John's University of Tanzania.
 
Soma mathayo 16:14 -21 ama soma mpaka aya ya 27 kisha soma maisha ya mitume wote uinjilishaji wao na vifo vyao wote. Kisha uje utuambie
Kama wewe uilishasoma hio mathayo na huo uinjilishaji unashindwa nni kuataja wakati gan kristu alianzisha hilo kanisa na ilikua wapi?
Kwa faida ya wanajamii weka hapa kila mtu aone
 
Rumi haijawahi kua Takatifu .

Mpaka Yesu anazaliwa, Rumi ilikua ikitawala kiserikali ( haikua na Dini).

Rumi hiyo ya kiserikali ilikua ina Sheria zake, tamaduni zake , mila zake , kama vile Kuabudu mungu Jua, Sanamu za wakuu wake, Miti ( huu unaotumika kwenye Christmas) kwakua ni mti uliokua unahimili hali ya ukame, ivo ukachaguliwa kama mungu wamimea, waliabudu mungu mwanamke n.k.

Yesu anazaliwa mpaka anaanza kazi zake, watu wakamfuata ,nao wakaitwa WAKIRSTO ..yaan watu wa Yesu Kristo. .

Yesu anasulubiwa, anaacha wanafunzi wanaichapa injili Dunia .

Aliyekua Papa wa Rumi ya kiserikali COSTANTINE , Baada yakuona mapambano dhidi ya ukrsito yameshindwa na kwamba Tamaduni za Roma zinaelekea kupotea.

aliamua mwenyewe ,kujiingiza katika Ukristo na kua KIONGOZI MKUU wakwanza wa Rumi kua Mkristo.

Ni katika huo Ukristo wake aloingia, ndio akafanikiwa baadae kwanza, kuitenga Jumapili kua ibada Dunia nzima( akijua kwa kuiabudu siku hiyo ya jumapili ya mungu Jua ), Kua Krismas ifanyike 25 /12 kuendelea kusherekea mungu wa mimea n.k n.k .

Sasa nn kilichotokea ???

Baada ya Rumi sasa kua na mamlaka mbili za kiserikali na Kidini , wapo wakrsto baadae waloona hapana, Rumi inaenda kinyume na Mafundisho ya Yesu .

Wakristo hao wakajitoa kwa Rumi nakuanzisha makanisa yao ,namiaka ilivyozidi kusogea wakazidi kujiondoa na kuanzisha makanisa ndo ambayo Leo yapo.

ROMA, HAIJAWAH KUA KANISA LA MITUME.

LABDA KAMA HUIJUI HISTORIA,

wazijua zama za Giza????

Ambapo Rumi hii , ilikua Wakristo zaidi ya million???..( gugo ).

Rumi iliua Wakristo mpaka mwaka 1798 ambapo Papa alichukuliwa mateka na Majeshi ya ufaransa , ndo ukawa mwisho wa mauaji ya Wakristo.

Mambo ni mengi , Ingia tafuta vitabu usome !!..... ROMA HAIJAWAH KUA KANISA LA MITUME.
Jibuni hii hoja na hayo mauaji ilitokeaje wakati Baba mtakatifu yupo
 
Hakuna sababu ya msingi mkatoliki kujitetea na hayo masanamu ya kanisani kila mtu anajibu kibinadamu tu wapi Yesu aliagizwa achongwe au wapi alisema tuchonge sanamu ya Nikita Maria sijui yoseph what is the relationship na ukombozi wetu
 
Vp ma. Pengo hamuwezi mpa utakatifu yule shoga wa pale st. Petro osterbay
Huna akili jikite kwenye hoja,huyo uliyemtaja una ushahidi upi ni shoga?
Unastahili kula ban,kwa bahati mbaya mods hawajui wanachokifanya humu.
@paws hawa wanaotweza utu wa viongozi wetu muwe wepesi kuwashughulikia.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
20211229_165853.jpg
 
Nawaza utakatifu anapewaje kiongozi kibinadamu tu?

Je, kuna ushahidi wa maandiko unaoonesha kuwa Papa anakuwa mtakatifu automatically?

Na Kama Roho mtakatifu anaongea na watu wake kipi wafundishe why wampangie cha kufundisha dunia nzima?
Utuache na mtakatifu wetu, hakuhusu. Mbona tukimuita Yesu ni Mungu hushangai? Sisi tuna utaratibu wetu ambao sio lazim uwe sawa na utaratibu wa dini yako.
 
Nawaza utakatifu anapewaje kiongozi kibinadamu tu?

Je, kuna ushahidi wa maandiko unaoonesha kuwa Papa anakuwa mtakatifu automatically?

Na Kama Roho mtakatifu anaongea na watu wake kipi wafundishe why wampangie cha kufundisha dunia nzima?

Haya mambo sio mambo ya Chadema na CCM. Ni magumu mno
 
Back
Top Bottom