Papa: Wanaokosoa baraka za wapenzi wa jinsia moja ni wanafiki

Papa: Wanaokosoa baraka za wapenzi wa jinsia moja ni wanafiki

Dah! Kila uchao vinyeo vyetu vinazidi kuwekwa hatarini, laiti ningekuwa sijapata watoto nisingethubutu hata kidogo, nitaificha wapi sura yangu baada ya miaka 10 ijayo? Eee Mwenyezi Mungu tunusuru na hii Sodoma na Gomora, ikikupendeza Mungu wetu tuepushe na kikombe hiki na mapenzi yako yatimie.
 
"Hakuna mtu atanipa kashfa ikiwa nitatoa baraka zangu kwa mfanyabiashara anayewanyonya watu, na hii ni dhambi kubwa sana. Lakini nitapewa kashfa ikiwa nitatoa kwa wapenzi wa jinsia moja, Huu ni unafiki"

Papa Francis amesema anaona kuna "unafiki" katika kukosolewa kwa uamuzi wake wa kuruhusu makasisi kuwabariki wapenzi wa jinsia moja.

Baraka za wapenzi wa jinsia moja ziliidhinishwa mwezi uliopita na hati ya Vatican iitwayo Fiducia Supplicans (Supplicating Trust), lakini ulikumbana na upinzani mkubwa katika Kanisa Katoliki, hasa kutoka kwa maaskofu wa Afrika.

Francis aliliambia jarida la Kikatoliki la Italia Credere kuwa "daima" anawakaribisha wapenzi wa jinsia moja na waliooana tena baada ya talaka kwenye sakramenti ya kuungama.

BBC Swahili
Agent wa kuzimu atawakokota wengi jehanum.
 
Kanisa liruhusu ndoa za mke zaidi ya mmoja huo upuuzi mwingine achane nao.
ingia kwenye uislamu utapata hiyo sheria kutoka mungu kuliko kusubiri uruhusiwe na papa ambae ni mtu Kama wewe ,na utambue hata akiruhusu ukifata bado una dhambi sababu utakua hujafata sheria ya mwenyezimungu utakua umefata sheria ya binadamu Kama wewe kwa maana sheria ya mungu habadiliki milele . umeambiwa usiongeze wala usipunguze na ndio maana kitabu cha uislamu hakibadiliki mpaka mwisho wa dunia . karibu kwenye uislamu utaweza kuoa wake zaidi ya mmoja na kanuni zake zipo toka enzi hizo na hazijabadilika na hazitobadilika sio kuoa tu wake wengi uwe na sifa pia sio unaowa halafu unawateza kwa kukosa uwadilifu
 
Hapo hata mimi nashangaa, marafiki wa Mungu walikuwa na Wake wengi na Mungu hakuwakataza, marafiki wa papa ni mashoga na hawakatazi. Hili kanisa katoliki lina kiongozi mlaaniwa kabisa.
Kama sio muislam ni wakati sahihi sasa wakua muislam

Wakati Allah kaamrisha watu waoe zaidi ya mke mmoja kwa mwenye uwezo na uadilifu kwa hao ataoa waoa

Shuleni wakatuletea mitaala yakijinga yakupinga ndoa za mke zaidi ya mmoja kwa kisingizio cha eti ni kinyume na haki za binaadam ila mbaya zaidi ukute kwasasa kuna mitaala watoto wanafunzwa kama asemavyo papa

Yanayotokea sasa ama kuendelea ni matokeo ya mafunzo walotupatia miaka zaidi ya 30 nyuma huko tukiwa mashuleni vyuoni na kadhalika

Na yanayosemwa sasa na mamba bado haijaonekana athari zake kamili athari zake kamili kama tutajaaliwa uhai uzima na afya miaka 30 au 20 ijayo ndio utaihisi ile wazi wazi kabisa

Uislamu ndio dini ya haki pakee hapa ulimwenguni
 
Hakuna mtu atanipa kashfa ikiwa nitatoa baraka zangu kwa mfanyabiashara anayewanyonya watu, na hii ni dhambi kubwa sana. Lakini nitapewa kashfa ikiwa nitatoa kwa wapenzi wa jinsia moja, Huu ni unafiki"
 
"Hakuna mtu atanipa kashfa ikiwa nitatoa baraka zangu kwa mfanyabiashara anayewanyonya watu, na hii ni dhambi kubwa sana. Lakini nitapewa kashfa ikiwa nitatoa kwa wapenzi wa jinsia moja, Huu ni unafiki"

Papa Francis amesema anaona kuna "unafiki" katika kukosolewa kwa uamuzi wake wa kuruhusu makasisi kuwabariki wapenzi wa jinsia moja.

Baraka za wapenzi wa jinsia moja ziliidhinishwa mwezi uliopita na hati ya Vatican iitwayo Fiducia Supplicans (Supplicating Trust), lakini ulikumbana na upinzani mkubwa katika Kanisa Katoliki, hasa kutoka kwa maaskofu wa Afrika.

Francis aliliambia jarida la Kikatoliki la Italia Credere kuwa "daima" anawakaribisha wapenzi wa jinsia moja na waliooana tena baada ya talaka kwenye sakramenti ya kuungama.

BBC Swahili
Kweli lakini!
Mbona kila familia zetu zina so called "black sheep"?! Tuko kimya na hatuwaaniki hadharani wala kupiga mayoe?!
Maybe he's right...
 
Huyu ataondolewa hivi karibuni
Hili zee limekosa hekima kabisa kabisa! Huyu naye ni khalifa wa Mtume Petro? Anakalia kiti cha Kefa huyu? Kwamba huyu atakalolifungua duniani na Mbinguni, kilipo Kiti cha Enzi litakuwa limefunguliwa? Ukisikia mambo haya umewafunulia watoto wachanga ukawaficha wenye hekima andiko linatimia kwa huyu mtu!
 
Huyu Papa (siyo papa mtakatifu ) nafikiri aliingia kwa Kazi maalumu ambayo ni kueneza na kuhalalisha ushoga katika kanisa katoriki. Anaupambania sana kama vile hakuna mambo mengine ya msingi yanayoikabili dunia na hata Hilo kanisa katoriki
 
Back
Top Bottom