Arch Barrel
JF-Expert Member
- Feb 1, 2024
- 434
- 1,126
Agent wa kuzimu atawakokota wengi jehanum.
"Hakuna mtu atanipa kashfa ikiwa nitatoa baraka zangu kwa mfanyabiashara anayewanyonya watu, na hii ni dhambi kubwa sana. Lakini nitapewa kashfa ikiwa nitatoa kwa wapenzi wa jinsia moja, Huu ni unafiki"
Papa Francis amesema anaona kuna "unafiki" katika kukosolewa kwa uamuzi wake wa kuruhusu makasisi kuwabariki wapenzi wa jinsia moja.
Baraka za wapenzi wa jinsia moja ziliidhinishwa mwezi uliopita na hati ya Vatican iitwayo Fiducia Supplicans (Supplicating Trust), lakini ulikumbana na upinzani mkubwa katika Kanisa Katoliki, hasa kutoka kwa maaskofu wa Afrika.
Francis aliliambia jarida la Kikatoliki la Italia Credere kuwa "daima" anawakaribisha wapenzi wa jinsia moja na waliooana tena baada ya talaka kwenye sakramenti ya kuungama.
BBC Swahili
ingia kwenye uislamu utapata hiyo sheria kutoka mungu kuliko kusubiri uruhusiwe na papa ambae ni mtu Kama wewe ,na utambue hata akiruhusu ukifata bado una dhambi sababu utakua hujafata sheria ya mwenyezimungu utakua umefata sheria ya binadamu Kama wewe kwa maana sheria ya mungu habadiliki milele . umeambiwa usiongeze wala usipunguze na ndio maana kitabu cha uislamu hakibadiliki mpaka mwisho wa dunia . karibu kwenye uislamu utaweza kuoa wake zaidi ya mmoja na kanuni zake zipo toka enzi hizo na hazijabadilika na hazitobadilika sio kuoa tu wake wengi uwe na sifa pia sio unaowa halafu unawateza kwa kukosa uwadilifuKanisa liruhusu ndoa za mke zaidi ya mmoja huo upuuzi mwingine achane nao.
Kama sio muislam ni wakati sahihi sasa wakua muislamHapo hata mimi nashangaa, marafiki wa Mungu walikuwa na Wake wengi na Mungu hakuwakataza, marafiki wa papa ni mashoga na hawakatazi. Hili kanisa katoliki lina kiongozi mlaaniwa kabisa.
Kweli lakini!
"Hakuna mtu atanipa kashfa ikiwa nitatoa baraka zangu kwa mfanyabiashara anayewanyonya watu, na hii ni dhambi kubwa sana. Lakini nitapewa kashfa ikiwa nitatoa kwa wapenzi wa jinsia moja, Huu ni unafiki"
Papa Francis amesema anaona kuna "unafiki" katika kukosolewa kwa uamuzi wake wa kuruhusu makasisi kuwabariki wapenzi wa jinsia moja.
Baraka za wapenzi wa jinsia moja ziliidhinishwa mwezi uliopita na hati ya Vatican iitwayo Fiducia Supplicans (Supplicating Trust), lakini ulikumbana na upinzani mkubwa katika Kanisa Katoliki, hasa kutoka kwa maaskofu wa Afrika.
Francis aliliambia jarida la Kikatoliki la Italia Credere kuwa "daima" anawakaribisha wapenzi wa jinsia moja na waliooana tena baada ya talaka kwenye sakramenti ya kuungama.
BBC Swahili
Hili zee limekosa hekima kabisa kabisa! Huyu naye ni khalifa wa Mtume Petro? Anakalia kiti cha Kefa huyu? Kwamba huyu atakalolifungua duniani na Mbinguni, kilipo Kiti cha Enzi litakuwa limefunguliwa? Ukisikia mambo haya umewafunulia watoto wachanga ukawaficha wenye hekima andiko linatimia kwa huyu mtu!Huyu ataondolewa hivi karibuni
Tulihabarishwa humu kuna delegation nzito itamtembelea. May be watarudi na nakala.Lini waraka wa Papa utasomwa katika makanisa yote nchi nzima?
Mtakatifu hawi dhaifuMtu mmoja anapotumika kuchafua taswira ya sehemu au watu fulani usihukumu watu wote bali chunguza huenda naye ni udhaifu wake
Papa ndiye boss wa hao kina kitimaKitima Ebu mtoeni huyu Mzee mana yawezekana ana shida pahala.Mfukuzeni asituletee
Papa hataki unaa🤠🤠🤠🤠🙌!