Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute' Haya ndiyo mambo tulikuwa tunataka Simba SC

Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute' Haya ndiyo mambo tulikuwa tunataka Simba SC

Mkuu Kichwa Kichafu Endelea kupata mateso.

Simba SC Ndo Mabingwa wa Nchi
Wawakilishi pekee kwenye mashindano ya kimataifa kwenye ukanda wote wa CECAFA. Nchi 8 zinawakilishwa na mnyama mmoja mkali sana. Dada zetu wa ukanda wa Jangwani na majirani zao (wenye derby yao) Wazee wa biskuti, wataiwakisha Tanganyika kwenye mashindano ya uhuru wa visiwa vya Zanzibar...

Tunawatakia kila la kheri watuletee kombe nyumbani. Nimeambiwa kombe litakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Temeke kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar...
 
Kwenye kupiga long pass kuna mambo mawili, inaweza kuwa mpokeaji ni wapi pa kupokelea hizo ndefu au mpigaji anapigaje..!

Kwa game ya Azam FC jana Kanoute amepiga long pass ambazo baadhi zilifika kwa Kapombe na zingine zilipotea

Ni wakati Kocha kulifanyia kazi
Nakupa changamoto 1,, kama hutojali jaribu kufuatilia hata mechi za nyuma utagundua nnachokisema, kwa role aliyonayo anapaswa kulifanyia kazi sana hiyo changamoto. Lakini naona anazidi kuimarika na ni mchezaji mzuri
 
Ni swala la muda tu ila Sakho ni Sadio mane mtupu
Hii kauli sio wa kwanza kusema...kuwa makini usitoe siri wasije wakamuumiza tena maana huyu mtoto ni chafya lazima ufumbe macho uipigapo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
WanaSimba tunaendelea kutembea mwendo wa Ngiri meno nje kuhusu hawa Vijana, Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute, kwa kadri wanavyozidi kuimarika na kuwa hatari sana Uwanjani, hongera sana Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC, haya ndo mambo tulikuwa tunasubiri, kwa WanaSimba

Pape Ousmane Sakho huyu kwa sasa ndo kiumbe mmoja hatari sana mwenye kuwang'oa wapinzani meno bila kutumia ganzi.

Kama namuona Luis Miquissone hivi kwa mbali, kwa uwezo wake wa kuondoka na Kijiji huku akiteleza mithiri ya samaki kambale pamoja na ubunifu wake na unyumbulifu uliothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika CAF.

Kwa sasa huyu kiumbe ni kero namba moja Tanzania, ukiachilia mbali Bernard Morrison wakili msomi mwenye uwezo wa kushinda kesi bila kusimama mahakamani.

Sadio Kanoute huyu ni kiumbe boksi to boksi, kiungo matata sana, mtaalamu mwenye kutembea dimba la kati kwa namna anavyotaka.

Huyu mtu sana, achilia mbali game dhidi ya Azam FC, alichofanya game dhidi ya Majirani Kutoka bonde la Jangwa kila mtu anajua, baada ya jina la Dokta kuzimika baada ya game, kama dawa iliyoisha muda wake.

Sakho na Kanoute haya ndo mambo ambayo tunataka Simba SC, hakika Azam FC wamekutana na dawa ya kuua Wadudu Wanaoruka na Kutamaa na hakika ukichagua Simba SC umechagua furaha Mutawalia, Simba SC Klabu Quality yenye kusakata kabumbu la Viwango vya CAF, Mabingwa wa Nchi, Klabu Kubwa na Bora Afrika.

Peter Banda tunasubiri uje kujibu mapigo haya ya Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute pomoja na kipaji chako cha kusakata kabumbu, bado nafasi unayo na umri unaruhusu pia.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.
Umeandika facts tup mkuu,

Simba, nguvu moja [emoji123]
 
Sakho mbona n mda tu alijitofautisha kuwa yeye n mchezaj wa namna gan toka wakiwa Morocco kule alikuwa anafunga sana
 
Limleta mada lina matatizo ya usimba sana
Hao wachezaji bora hata mkandala wa dodoma jiji, hata mbeya kwanza hawapati namba
 
Ule msuti wa Sakho jana dhidi ya Azam FC uliogonga mwamba, yaani golikipa angeruka juu zaidi kisha akapangua lazima angekata network kama suti la Kanoute dhidi golikipa wa Timu ya bonde la Jangwa
Azam bwana timu ya kindugu ukiwa mZnz bari afu ostadh unapata namba...imekosa watu wa mpirampira angalia magolikipa wao hasa yule namba 2.
 
Sakho toka mwanzo alionyesha ni mchezaji mzuri lakini hapo katikati alipotea kabisa. Nafikiri majeraha aliyoyapata mwanzoni mwa ligi na kuzoea mazingira ndio vilimpa shida.

Ila ile spidi ya Sakho tena akiwa na mpira mguuni hii itakuwa ni shida nyingine kwenye ligi ya Tanzania. Kwa jinsi ninavyowajua mabeki wa timu za kitanzania (Yondani, Nyosso, n.k.) itabidi viongozi wa Simba wawe wanalalamika mapema kabla mpira haujaanza ili marefa wawe ättention" vinginevyo kila wakati Sakho atakuwa majeruhi.
 
Limleta mada lina matatizo ya usimba sana
Hao wachezaji bora hata mkandala wa dodoma jiji, hata mbeya kwanza hawapati namba
We umelewa vyura wa pale Jangwani ndo maana ukaandika huu upoyoyo.

Pape Ousmane Sakho is a talented player.

Pape Ousmane Sakho is very skillful and fact. His play is much similar to Sadio Mane.
 
Back
Top Bottom