Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute' Haya ndiyo mambo tulikuwa tunataka Simba SC

Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute' Haya ndiyo mambo tulikuwa tunataka Simba SC

Ila kuna watu hawajui mpira kabisa mim binafs huyo sakho na kanuote niliwakubar siku ya kwanz tu na nikaamin ni suala la muda tu...Mchezaj utamjua tu akiwa na mpira au akiwa hana mpira,.Hyo sakho ana mikimbio hatar sana.. Mtu anayejua mpira akiupata tu mpira unajua huyu fund tumpe muda
 
Sakho ni mchezaji bora wa msimu wa 20/21 kwenye ligi kuu ya Senegal, akiwa na mabao sita na assts 6 kwenye Ubingwa wao Klabu ya Teungueth.

Na saaa yupo kwa Mabingwa wa Nchi na Wawakilishi wa Kimataifa, huko kwenu nani anasifa hizo? Huko alikotoka?
Iyo league au Bonanza?

Mpira wa senegal bora zanzibar
 
Nyie mikia siku ile ya derby hao wote si mliwatoa nje?na mkaanza kulalamika kua viongozi wamesajiri vitoto...Yanga hii hebu ipe heshima yake ...alaa huna adabu hata kidogo.
Nyie mikia siku ile ya derby hao wote si mliwatoa nje?na mkaanza kulalamika kua viongozi wamesajiri vitoto...Yanga hii hebu ipe heshima yake ...alaa huna adabu hata kidogo.
unazungumzia hii hadi mdaka mishale alikuwa hoi kwa shuti la sadio kanoute

D450C7CE-F58A-4726-AC2C-FA4A7154EB78.png
 
Wapi mashabiki wenye maono walilalamika?

Hivi Kanoute alipozima zile tambo za akina Aucho na Faisal pale katikati ya dimba hukuona?

Au lile shuti aliopiga Kanoute golikipa wenu akakata Network na kutibiwa kwa dakika kadhaa hukuona?
😂😂😂

2F91DB32-D973-4FB4-BF6A-27349F91DADE.png
 
WanaSimba tunaendelea kutembea mwendo wa Ngiri meno nje kuhusu hawa Vijana, Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute, kwa kadri wanavyozidi kuimarika na kuwa hatari sana Uwanjani, hongera sana Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC, haya ndo mambo tulikuwa tunasubiri, kwa WanaSimba

Pape Ousmane Sakho huyu kwa sasa ndo kiumbe mmoja hatari sana mwenye kuwang'oa wapinzani meno bila kutumia ganzi.

Kama namuona Luis Miquissone hivi kwa mbali, kwa uwezo wake wa kuondoka na Kijiji huku akiteleza mithiri ya samaki kambale pamoja na ubunifu wake na unyumbulifu uliothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika CAF.

Kwa sasa huyu kiumbe ni kero namba moja Tanzania, ukiachilia mbali Bernard Morrison wakili msomi mwenye uwezo wa kushinda kesi bila kusimama mahakamani.

Sadio Kanoute huyu ni kiumbe boksi to boksi, kiungo matata sana, mtaalamu mwenye kutembea dimba la kati kwa namna anavyotaka.

Huyu mtu sana, achilia mbali game dhidi ya Azam FC, alichofanya game dhidi ya Majirani Kutoka bonde la Jangwa kila mtu anajua, baada ya jina la Dokta kuzimika baada ya game, kama dawa iliyoisha muda wake.

Sakho na Kanoute haya ndo mambo ambayo tunataka Simba SC, hakika Azam FC wamekutana na dawa ya kuua Wadudu Wanaoruka na Kutamaa na hakika ukichagua Simba SC umechagua furaha Mutawalia, Simba SC Klabu Quality yenye kusakata kabumbu la Viwango vya CAF, Mabingwa wa Nchi, Klabu Kubwa na Bora Afrika.

Peter Banda tunasubiri uje kujibu mapigo haya ya Pape Ousmane Sakho na Sadio Kanoute pomoja na kipaji chako cha kusakata kabumbu, bado nafasi unayo na umri unaruhusu pia.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.
Kushoto una sakho kulia ina morison namba 10 una ********! Boks to boks una kanoute.... kazi ipo.....
Huyu sakho ni miquisson mwingine...
 
Back
Top Bottom