Parade ya pamoja us na russia red square moscow

Enkaly

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2014
Posts
307
Reaction score
428
moja moja.jpg

Kutokana na picha hiyo hapo juu dunia inapata somo gani kwa USA kushiriki parade ya pamoja ya victory day may 9 katika viwanja vya red square moscow miaka michache iliyopita?
 
Victory day nchini Urusi ni siku maalumu ya kusherehekea na kukumbuka ushindi wa USSR na nchi washirika katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1945 dhidi ya Ujerumani ya Adolf Hitler na chama cha NAZI.

Nchi washirika upande wa USSR zilizoshinda WW2 ni pamoja na Marekani ambayo ilitoa misaada mbalimbali ya kijeshi na kiraia kwa USSR iliyoiwezesha USSR kukabiliana na uvamizi wa Hitler wa mwaka 1941.
 
Hakuna rafiki au adui wa kudumu.
 
Watakupinga kuwa USSR haikuwasaidiwa na US. Kuna watu wanaona US ni mtu wa kawaida yaani, huyu jamaa ni mtata toka kitambo na anajiweza kitambo tu.
 
Sio kusaidia kwa namna anavyotaka kutuaminisha hapa,kwwnye vita kubwa kama ile kila Nchi huwa ina take sides.

Ni kama ilivyo sasa zinapopigwa kura kule Ummoja wa mataifa,katika Vita ya 2 USSR & USA wote walikuwa na adui mmoja Germany-na hiyo ni baada ya Germany kutangaza vita dhidi ya USA.
 
Wanaopinga kuna mawili: hawajui historia, ama wanaijua hiyo historia ila hawataki kukubaliana na huo ukweli kwa makusudi tu pengine kwa sababu ya uhasama wao na Marekani.

Ukweli ni kwamba, bila ile Lend-Lease Act ya Marekani ya mwaka 1941, leo pengine tungekuwa tunaongea masuala tofauti kabisa, maana majeshi ya Hitler yalikuwa tayari yameshakanyaga Moscow.
 
Kwa hiyo KUMBE marekani alisaidia ili asivamiwe,kumbe RUSSIA kiboko akasaidiwa ili amsaidie.basi sawa
 
Hadi leo USA na Russia ni marafiki. Kwani wana uadui gani? Si kuna balozi pande zote?
 
USA na RUSSia Ni washkaji wanaojuana.

We jinchanganye Ile kwako.

Zelensky kajichanganya akiingiza nchi matatizoni[emoji1787]
 
Wanaopinga kuna mawili: hawajui historia, ama wanaijua hiyo historia ila hawataki kukubaliana na huo ukweli kwa makusudi tu pengine kwa sababu ya uhasama wao na Marekani.

Ukweli ni kwamba, bila ile Lend-Lease Act ya Marekani ya mwaka 1941, leo pengine tungekuwa tunaongea masuala tofauti kabisa, maana majeshi ya Hitler yalikuwa tayari yameshakanyaga Moscow.
Majeshi ya Hitler yalikanyaga Moscow na yalikua yakielekea kushinda, Hitler akamega jeshi kupeleka front nyingine,ndipo mkong'oto ulipoanzia
 
Back
Top Bottom