The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mkoa wa Arusha Cecilia Daniel Paresso Cecilia Paresso amesema ahadi ambazo alizitoa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa atatekeleza ndani ya siku 100 tayari ameanza kuzitekeleza ikiwemo mpango wa bima ya afya kwa wote na mikopo kwa wajasiriamali.
Akizungumza Februari 2, 2026 akiwa jijini Arusha katika mkutano wa hadhara wa mapokezi ya mbunge jimbo la Arusha Mjini(CCM) Paul Makonda ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
"Leo ana siku 90 yuko ofisini takribani mambo 10 aliyoahidi watanzania anaenda kuyatimiza"
Amesema katika kutekeleza mpango wa bima ya afya kwa wote tayari Rais Samia ameanza utekelezaji huo kwa kuanza na makundi maalum ambapo usajili kutambua makundi hayo umeshaanza kufanyika. Kwa upande wa ahadi ya kutenga bilioni 200 kwa wafanyabishara wadogo, Paresso amesema usajili wa makundi ya wanufaika umeshaanza kufanyika katika Halmashauri zote nchini huku akitoa wito kwa makundi hayo kuchangamkia fursa na mikopo itakapotoka iwafaidishe.
Aidha ametumia mkutano huo kumpongeza Makonda kwa kuchaguliwa na wanaarusha na kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa huku akikishukuru chama chake cha CCM kwa kumuamini na kupendekeza jina lake kuwa Mwenyekiti wa Bunge ambapo alipitishwa na kushika nafasi hiyo.