Nyota wa PSG amesherehekea siku ya kuzaiwa ya dada yake akiwa pamoja na mchumba wake Bruna Marguezine.
Majeraha yanayomkabili mshambuliaji huyo nyota raia wa Brazil hayakumzuia kutekeleza masuala yake ya kijamii.
Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa klabu ya muziki ya usiku nchini Brazili ambapo dada wa Neymar aitwaye Rafaella, alikuwa anatimiza miaka 22.
Neymar alionekana akichechemea mguu, huku akiwa na magongo yake pamoja na mpenzi wake aliyekuwa akimsaidia kwa ukaribu.
Nyota huyo amekuwa akijaribu kufanya mazoezi ya hapa na pale ili kujiweka fiti iwapo anaweza kurejea dimbani kwa ajili pia ya mashindano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni mwaka huu.
Hata hivyo, kumekuwa na taarifa kuwa baba yake mzazi ameiomba PSG kutopandisha dau dau lolote ili kumuuuza kwa klabu ya Real Madrid.