Paris Saint-Germain Special Thread

Paris Saint-Germain Special Thread

Tetesi

Miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain inamtaka Antonio Conte kuwa meneja wao.

Vinara hao wa The Ligue 1 wanamnyatia pia meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino.
 
Barcelona, Paris St-Germain na Real Madrid zinataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah , 25 kwa dau la uhamisho litakalovunja rekodi la £200m. Raia huyo wa Misri amefunga mabao 28 katika ligi ya Uingereza msimu huu. (Sun)
 
Nyota wa PSG amesherehekea siku ya kuzaiwa ya dada yake akiwa pamoja na mchumba wake Bruna Marguezine.
Majeraha yanayomkabili mshambuliaji huyo nyota raia wa Brazil hayakumzuia kutekeleza masuala yake ya kijamii.


Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa klabu ya muziki ya usiku nchini Brazili ambapo dada wa Neymar aitwaye Rafaella, alikuwa anatimiza miaka 22.

Neymar alionekana akichechemea mguu, huku akiwa na magongo yake pamoja na mpenzi wake aliyekuwa akimsaidia kwa ukaribu.
Nyota huyo amekuwa akijaribu kufanya mazoezi ya hapa na pale ili kujiweka fiti iwapo anaweza kurejea dimbani kwa ajili pia ya mashindano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni mwaka huu.


Hata hivyo, kumekuwa na taarifa kuwa baba yake mzazi ameiomba PSG kutopandisha dau dau lolote ili kumuuuza kwa klabu ya Real Madrid.
 
MABOSI wa Paris Saint-Germain wameshakubaliana na hali halisi kwamba kocha wanayemsaka Luis Enrique atatimkia Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Antero Henrique alikuwa na mpango wa kumvuta kocha huyo wa zamani wa Barcelona kwenye kikosi chake na kumpiga chini Unai Emery.
Lakini taarifa zinadai bosi huyo ameshaambiwa kila kitu kuwa Enrique amekubali dili la kwenda kuinoa Chelsea na kinachosubiriwa ni msimu tu umalizike akarithi mikoba ya Antonio Conte.
Kutokana na hilo, PSG sasa itakuwa na nafasi ya kumchukua Conte kama itahitaji huduma yake, huku taarifa za karibuni zikidai wababe hao wa Ufaransa wamekuwa wakipiga hesabu za kuinasa huduma ya Mtaliano huyo ili akawafanye kuwa bora zaidi na kushindana kwenye michuano mikubwa kama ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Follow this link to join my WhatsApp group: WAZEE WA KUWEKA MIZIGO
Hili Group ndo lile mtu akiamua kutoa watu anatoa toa tu? linaboa sana... mtu anapojoin si lazima acomment same day wakat topics zilizo mezani hana cha comment ila linatokea puuz moja nyuma linasema nafuta watu wasiocomment hata tukibaki watatu tunaochat ndo nataka... sasa kama unataka waatu wakuchat nao mnasambaza link ya nn
 
32859257_10156653389223598_637290468605952000_n.jpg
 
Wakuu habari zenu
Naona ufalme wa ufaransa ni wenu tu
Kama juve na italy
 
Jana PSG wamepata kibonde. Neymar katupia Hatrick

Jana nimekaa na shabiki WA liver akaiponda sana hii timu,nikamwambia kuwa wamedroo na Napoli hawa akanijibu kuwa kwan napoli anampira gani subiri uone ninavyompiga Napoli goal 4...!
Nadhani mpka sasa majibu anayo!!
 
Back
Top Bottom