Parking fee kamata kamata

Wapendwa natumaini hamjambo.
Kama kuna mtu anadaiwa parking ya gari inayozidi 10,000. Lipa kabla ya saa nne leo, vinginevyo ukikamatwa gari linapelekwa godown na unalipa laki nne.! Hiyo ni kuanzia leo 04/09/2023
Unaangaliaje madeni?
 
Hapo sasa haijulikani kama ni kwa wote ama la ila kwa jinsi nchi hii watu wasivyotumia akili wanaweza kukomaa na kigezo cha kuzidi 10,000/= tu sasa mimi nasubiri wanikamate nipambane nao
 
Hapo sasa haijulikani kama ni kwa wote ama la ila kwa jinsi nchi hii watu wasivyotumia akili wanaweza kukomaa na kigezo cha kuzidi 10,000/=
Kabisa na hiyo hasa ndio hofu yangu. Maana hii nchi kila kauli huwa ni fursa. Kwa upeo mdogo wa hao watendaji wao sidhani kama watataka kusikia kipengele cha muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…