Parking fee kamata kamata

Wanapiga picha hata gari zilizo gereji za karibu na barabara, wakati garama ya eneo inatakiwa ilipwe na mwenye eneo.
 
Lakini zile parking mbele ya maduka yao ni kweli za serikali ya mitaa, zamani zilikuwa na hizi machine

View attachment 2738802
Unafikiri hatutaki kulipa kodi shehe, shida ni pale utaratibu unapokuwa wa upendeleo na adhabu isiyo endana na kinachodaiwa.
WASANII juzi wamekopeshwa milioni 40 kila mmoja na hawajarudisha na hawatarudisha na kila siku wapo wakula k-vant wavuvi camp hakuna wa kuwauliza na wanaalikwa kwenye sherehe za serikali na kulipwa mamilioni, ila mnyonge aliyepaki Pembezoni mwa duka la majeneza pale muhimbili kununua jeneza la mke wake aliyefariki Mwaisela unakamata gari lake! Daah!
 
Eti unawapa hela wasanii [emoji1]

Ova
 
Unadai Tsh. 16,000 gari inakamatwa kabla ya muda wake wa mwisho wa kulipa deni, alafu ulipishwe laki nne. Msiamini uchawi upo, ukitokea mtu unalogea wanawe, atapike laki nne zangu, maana kuuguza ni fedha.
 
Hapo sasa haijulikani kama ni kwa wote ama la ila kwa jinsi nchi hii watu wasivyotumia akili wanaweza kukomaa na kigezo cha kuzidi 10,000/= tu sasa mimi nasubiri wanikamate nipambane nao
Upambane na nani? Unafikiri Kuna mtu atakayekusikiliza ?

Hi nchi imeshapoteza muelekeo Kila mtu anafanya anachojisikia

Maeneo ya kariakoo Kuna watu wanavaa suruali nyeusi na shati jeupe kazi Yao kukamata Magali sijui ndio akina nani hawa

Nakumbuka JPM alipiga marufuku mtu ambaye sio polisi kufanya kazi za kipolisi ila Kwa Sasa wamerudi Kwa kasi wamezagaa Kila mtaa
 
Nitatumia fact sitakubali kupelekwa godown na kuchajiwa kizembe never
 
Wapendwa natumaini hamjambo.
Kama kuna mtu anadaiwa parking ya gari inayozidi 10,000. Lipa kabla ya saa nne leo, vinginevyo ukikamatwa gari linapelekwa godown na unalipa laki nne.! Hiyo ni kuanzia leo 04/09/2023


Kwa watu ambao hawajui sheria na taratibu, walinifanyiaga huo ujinga miaka ya nyuma hawatasahau maisha yao yote maana walinitafuta mpaka kwa Baba Mzazi.
 
Kwa watu ambao hawajui sheria na taratibu, walinifanyiaga huo ujinga miaka ya nyuma hawatasahau maisha yao yote maana walinitafuta mpaka kwa Baba Mzazi.
Safi sana ndio raha ya kujua sheria kamwe huwezi kuonewa hovyo hovyo
 

Hawa wazee wa Wrong Parking wananjaa balaa kama mchwa. Sema ukiwa mwoga watakusumbua sana.[emoji23][emoji23]
 
Hapa inaonesha ulipaki wapi na kwa muda gani:Termis Web System
 
Ina makosa mno wala usifuatishe, nenda barbarani wale wa vimashine watajie namba ama traffic.
Ni kweli, unaweza kukuta umewekewa umepaki sehemu ambayo hujawahi hata kupaki. Mimi mwenyewe nimeangalia kunasehemu naangiziwa napaki kila siku na eneo lenyewe liko Mwanza wakati mimi nipo dar es salaam.
Ukitaka uone ulipaki wapi, ingia kwenye website ya tarura(Termis)
Ingia dirisha la lipia na ingiza namba yako ya gari na ku search; Itakuanyesha kiasi unachodaiwa. Ukitaka uone ulipaki wapi unabonyeza kitufe kilicho andikwa Tiketi na itakuletea mkeka wote wa sehemu ulizopaki na haujalipia.
 
Najaribu ile *152*01# haifanyi kazi, nimedownload hiyo GePG nakuta nina deni aiseee.
 
Kawe beach na ukimya wote ule ukipark wanakuandikia fasta
 
Mimi walishanisumbua sana.
Siku hz nkipaki namuangalia kwanza nijue alipo, then namchana wazi kua anisubirie tumalizane asihangaike kupiga hyo picha. Nkitoka nampa 200 au jero ya maji nasepa
Jero kwa muda gani???[emoji1787][emoji1787][emoji1787]maana dar ni kuanzia afu 2 ndo mtu anakubalii hapo unakaa siku nzimaaa..
 
Nchi za wenzetu sehemu za parking za kulipia miundombinu yake yenyewe mizuri,hata ukitoa pesa hujuti
Ila kwa tanzania ni uhuni uhuni tu
Wao wanachofikiria ni kutoza tu pesa
Mambo ya usalama wa gari na Mali zako hayawahusu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…