Parking kando ya barabara ni wizi wa mchana kweupe, maana yake wanataka watu wawe wanabeba magari mgongoni wakitaka kuingia mahali kununua bidhaa au kupata huduma? nimekaa majuu kuna street parking, watu wanapaki magari kando ya barabara mitaani kwenye maeneo yalipo makazi yao hata mwaka mzima na hakuna wanacholipia. Utaratibu wa kulipia parking unatakiwa uwepo kwenye maeneo maalumu yaliyojengwa kama maegesho na halmashauri au watu binafsi kama ilivyo mlimani city, siyo kando ya barabara zilipo huduma na biashara.........watu wame park eneo la bar wanapata vinywaji, mtu anakuja kutoza parking, hii haiwezi kuwa haki.