Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanaJF,
Ni mimi tena, na nimeamka salama. Nimechelewa kuingia kazini leo, ila Mungu ni mwema nimeanza. Kuna habari njema naitegemea kutoka sehemu (ntawajuza mambo yakiiva). Ngoja tuendelee kuongea kupoteza pressure...
Umewahi kushangaa kwa nini kuna watu wanapiga hatua, hata endapo wana kipato kidogo. Na wengine wanakwama, pamoja na kujipatia 5m+ kwa mwezi? (Mdada wangu wa kazi ana viatu vingi kuniliko, haha). Well, leo nimekutana na Parkinson's law of money, ambayo tutaijadili kwa ufupi hapa.
Sheria ya Parkinson, iliyoanzishwa na Cyril Northcote Parkinson mnamo 1955, inasema kuwa:
Yaani, ukijiambia kuwa ntalima hili shamba kwa lisali moja, itakuwa hivyo. Au siku 3, utapata wasaa wa kugawa nguvu hadi siku 3 zitimie. (Ukitaka kufanikiwa, jaribu kuapply sheria hii katika utendaji wako wa kazi. Bana muda wako, utakwenda haraka.).
Kanuni hii pia sura ya kiuchumi, na inajulikana kama Sheria ya Parkinson ya Pesa:
🔺 🏢 Bajeti za Biashara – Idara inapopewa bajeti ya Tshs 20,000,000, itatafuta njia zote za kuitumia pesa zote, hata kama ingeweza kufanya kazi hiyo kwa Tshs 8,000,000.
🔺 🏛️ Matumizi ya Serikali – Serikali au mashirika hutumia bajeti yote ili kuhalalisha maombi ya pesa zaidi mwaka unaofuata.
✅ 📉 Kubali "Kufulia" Kwa Muda Fulani – Kawaida maisha yanapopanda, matumizi huongezeka. Utaitwa "bosi" na majirani/marafiki wanaolenga ulicho nacho. Jifanye kana kwamba umefulia, huku ukitathmini cha kufanya (nilijifunza kwa mama mzazi alipopokea pension yake).
✅ 🤔 Tathmini Kila Gharama – Ule msemo wa "tumia pesa zikuzoee" hautakusaidia. Ushindi upo kwenye hifandi/akiba, sio matumizi.
✅ 📊 Wekeza Kwenye Mali, Si Vitu– Elekeza pesa zako kwa vitu vinavyoongeza thamani yako ya kifedha badala ya matumizi yasiyo na faida.
Nakuombea hali yako ya fedha iimarike mwaka huu.
Ni mimi tena, na nimeamka salama. Nimechelewa kuingia kazini leo, ila Mungu ni mwema nimeanza. Kuna habari njema naitegemea kutoka sehemu (ntawajuza mambo yakiiva). Ngoja tuendelee kuongea kupoteza pressure...
Umewahi kushangaa kwa nini kuna watu wanapiga hatua, hata endapo wana kipato kidogo. Na wengine wanakwama, pamoja na kujipatia 5m+ kwa mwezi? (Mdada wangu wa kazi ana viatu vingi kuniliko, haha). Well, leo nimekutana na Parkinson's law of money, ambayo tutaijadili kwa ufupi hapa.
Sheria ya Parkinson, iliyoanzishwa na Cyril Northcote Parkinson mnamo 1955, inasema kuwa:
"Kazi huongezeka ili kujaza muda uliotengwa kwa ajili yake."
Yaani, ukijiambia kuwa ntalima hili shamba kwa lisali moja, itakuwa hivyo. Au siku 3, utapata wasaa wa kugawa nguvu hadi siku 3 zitimie. (Ukitaka kufanikiwa, jaribu kuapply sheria hii katika utendaji wako wa kazi. Bana muda wako, utakwenda haraka.).
Kanuni hii pia sura ya kiuchumi, na inajulikana kama Sheria ya Parkinson ya Pesa:
💸 "Matumizi huongezeka kulingana na kipato."
🔍 Inavyofanya Kazi
Unapopata pesa zaidi, utajaribiwa kutumia pesa zaidi badala ya kuweka akiba au kuwekeza. Unaweza kujikuta ukinunua vitu visivyo vya lazima au kupandisha status za maisha, na hivyo ukabaki kwenye hali yako ya kifedha isiyoridhisha.📌 Mifano ya Namna Sheria Hii Inavyofanya Kazi
🔺 Mfumuko wa Mtindo wa Maisha – Unapata mshahara mkubwa, lakini badala ya kuweka akiba, unanunua gari kali (nje ya uwezo wako) au kuhamia kwenye nyumba kubwa zaidi ya kodi ya juu.🔺 🏢 Bajeti za Biashara – Idara inapopewa bajeti ya Tshs 20,000,000, itatafuta njia zote za kuitumia pesa zote, hata kama ingeweza kufanya kazi hiyo kwa Tshs 8,000,000.
🔺 🏛️ Matumizi ya Serikali – Serikali au mashirika hutumia bajeti yote ili kuhalalisha maombi ya pesa zaidi mwaka unaofuata.
🛑 Jinsi ya Kuepuka Mtego wa Sheria ya Parkinson ya Pesa
✅ 💰 Jiwekee Akiba Kwanza – Kabla ya kutumia pesa zako, jilipe kwanza. Weka sehemu fulani kwa ajili ya akiba na uwekezaji.✅ 📉 Kubali "Kufulia" Kwa Muda Fulani – Kawaida maisha yanapopanda, matumizi huongezeka. Utaitwa "bosi" na majirani/marafiki wanaolenga ulicho nacho. Jifanye kana kwamba umefulia, huku ukitathmini cha kufanya (nilijifunza kwa mama mzazi alipopokea pension yake).