Paroko Msaidizi wa Parokia ya Magomeni (Dar), Christopher Fosudo afukuzwa nchini, Askofu Mkuu atoa maagizo

Yaleyale ya kina father Privatus karugendo. Alifukuzwa na kanisa kwa ajili ya aina ya mafundisho yake kwa waamini. Kwa mfano alikuwa akitetea matumizi ya condom wakati kanisa lilipinga kwa nguvu zake.

Aende tu. Kama kanisa limeona hafai, basi hamna namna aende tu.
 
Kanisa halina fungu la msamaha tena?
Fuatilia kisa cha Galileo Galilei aliyesema dunia ni duara huku kanisa Vaticano likiwa na msimamo dunia ni bapa, halafu fuatillia kisa cha Martin Luther kujitenga na Vatinano na kuanzisha Lutheran church huku akitowa sababu 105 kama sikosei.
 
Kisa? Au tuwaachie wenyewe?

Eidha anafanya biashara za magendo, wake za watu au ana kiburi akiagizwa au kala hela za taasisi?
Vyote hapo juu vyaweza kuwa majibu sahihi.
 
Sio uhamiaji ndio wenye uwezo wa kumfukuza mtu nchini? Angemsimamisha kazi na uhamiaji ifanye kazi yake.
Bila Kanisa Catholic kumdhamini, asingepewa visa ya kufanya kazi na kuishi Tanzania. Mdhamini wako akijitoa automatically na visa finito, basta
 

Kuna tetesi fulani fulani tangu yule padre alokutwa kafa mazingira y kutatanisha!!! any way ngoja niishie hapo kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…