Paroko Msaidizi wa Parokia ya Magomeni (Dar), Christopher Fosudo afukuzwa nchini, Askofu Mkuu atoa maagizo

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Magomeni (Dar), Christopher Fosudo afukuzwa nchini, Askofu Mkuu atoa maagizo

Rome acheni iitwe Rome..

#MaendeleoHayanaChama
Taasisi ngumu, isiyo yumba na imara tangu enzi za akina Martin Luther na Papa Clement V11 alipo mnyima kibali cha kuoa mfalme wa Henry V111 kumuona Catherine of Argon karne ya 16. Henry akachukia na kujitoa ktk Uka-toliki na kuanzisha Church of England ( Anglican). NA Catholic haikuyumba.
 
Kanisa imeshapata ripoti kuhusu mauaji wa mapadri yenye utata?

Wafuatilie haya mambo
 
Atakuwa alikutwa kwenye mabweni ya ma sista na aliingia huko akiwa kavalia kama sista
 
Sio uhamiaji ndio wenye uwezo wa kumfukuza mtu nchini? Angemsimamisha kazi na uhamiaji ifanye kazi yake.
Baba Askofu anajua sababu maana yeye ndiye mwenye jimbo lake ukiwa unapewa Upadre wanakili kutii kauli za Askofu so hakuna wakupinga hapo
 
Mtawalaumu bure hao mapadri, muwaruhusu tu kuoa. Isije kuwa alikuwa anakula mke wa mtu.
 
Taarifa ikufikie kuwa hili ndilo tamko lililotolewa na Chancellor Fr. Vincent Mpwaji wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, japokuwa kisa hakijatajwa lakini hizi ndiyo taarifa za uhakika kutoka katika kanisa hilo, jisomee mwenyewe uone

Inasomeka hivi...

Waheshimiwa Mapadre Wote,
Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

YAH: TAARIFA MUHIMU KUHUSU PD. CHRISTOPHER FOSUDO

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu.
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwaichi OFMCap anatoa taarifa kwamba Padri Christopher Fosudo kutoka Nigeria ambaye alikuwa anahudumu hapa Jimboni kama Paroko Msaidizi wa Parokia ya Magomeni, hatakiwi tena kuwepo hapa Jimboni Dar es Salaam. Hivyo Askofu Mkuu amemuagiza Padri Fosudo anudi nchini kwake Nigeria.

Fr. Vincent Mpwaji,
Chancellor- Jimbo Kuu la Dar es Salaam

KUNA KITU HAKIPO SAWA, HADI ANAFUKUZWA
 
They should have told us also what wrong he had done to deserve such punishment of church sending him back to his country.
Watuambie sisi ili iweje. Hiyo ni barua ya kiofisi, mwandishi katoa taarifa kuhusu hiyo barua, kanisa haliwajibiki kuambia umma chochote. Wahusika wametaarifiwa na huenda mtaarifiwa/mhusika amepewa barua kumueleza kwa nini huduma zake hazihitajiki parokiani.
 
Ilikuwa lazima atutangazie? Jinsi alivyomleta bila kutangaza, angemrudisha hivyohivyo
Tofautisha kanisa na mwandishi wa habari. Hizi habari tumezipata toka mwandishi na siyo vinginevyo. Kanisa halihusiki na hizo habari kuingia mtandaoni.
 
Kuna tetesi fulani fulani tangu yule padre alokutwa kafa mazingira y kutatanisha!!! any way ngoja niishie hapo kwanza
Sasa kama yumo kwenye hiyo tetesi...hiyo si Murder Mkuu.....wanamuachiaje sasa aondoke?
 
Back
Top Bottom